Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Habari waungwana,
Ndoto ni kitu ambacho ima humpa mtu faraja au kunyima raha kabisa inategemea sana na misingi ya mhusika kwa namna anavyozichkulia ndoto.
Lakini huku mtaani, kazini na hata kwenye mitandao hasa JamiiForums naona kasi ya watu kuleta ndoto na kuomba zitafsiriwe imekuwa kubwa pengine kuliko wakati mwingine wowote.
Kwa utafiti wangu mdogo jamii yenye kipato au yenye maisha magumu huwa wanapoteza muda sana kuhangaikia ndoto, au mtu aliekuwa na hali fulani ikabadilika ima kuwa juu au chini basi huanza kuota ndoto na hata kumfanya afurahie au aishi kwa hofu.
Sasa najiuliza inawezekana ndoto hizi kuletwa kwa wingi ni dalili ya maisha kuwa magumu au mazuri huko kitaani?