Mwanamume atabaki kuwa mwanamume, hii haijalishi kuwa ana kipato kidogo ama kikubwa, anazidiwa na mwanamke ama la ila inategemea unaendeshaje familiya yako. Kama huyo ni mkeo mnatakiwa kuwa kitu kimoja mishahara yenu muiweke pamoja mpange mikakati kwa pamoja na kwa umoja japo hii inategemea tangu mwanzo mlianzaje mahusiano yenu ya kimapenzi na kifedha. A man is not a provider but a guider hivyo hata kama mkeo anakuzidi kipata anaweza kukuheshimu lna kuuleta mshahara wake wote mkaupanga kama hii fedha ni kwa ajili ya kusomeshea watoto, hii matumizi nyumbani, hii yako mama, hii yangu baba, hii ya dharula, hii akiba na hii ku-support ndugu na jamaa. Mambo yanakwenda vizuri ila kama ndoa imetawaliwa na ubinafsi, usaliti na kiburi basi mnatakiwa kubadili mtazamo na kuanza kushirikiana. Upandacho ndicho uvunacho hivyo nashauri ni bora mtu achukuwa mda kumpata mke anayemfaa kuliko kuangalia juu juu tu na kuopoa mke, maisha hayana kanuni hubadilika wakati wowote hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kabla ya hatari.