Ndoa za zamani na sasa!!!

Ndoa za zamani na sasa!!!

nkungwe123

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
444
Reaction score
95
1. Zamani wanaume walioa na wanawake waliolewa. Kila mmoja alitimiza majukumu yake vyema na kwa staha kubwa. Siku hizi watu wanaoana. Majukumu yote ni ya wana ndoa bila kujali jinsia.
2. Zamani wanawake walikuwa wasikivu kwa waume Zao. Utii ulikuwa juu. Siku hizi wanawake wabishi kinoma. Wanatafuta tuzo za ubishi ktk familia.
3. Zamani wanawake walivaa kanga, sketi, gauni n.k siku hizi ni mwendo wa suruali za kubana na nguo za ajabu ajabu.
4. n.k
Unadhani kuoana kwa sasa ndio kunawafanya wawe wabishi kwa waume zao?
Toa maoni yako tafadhari..
 
Zamani ndoa zinadumu hadi kifo...siku hizi unaoa leo jumatatu ikifika Ijumaa mshaachana
 
Elimu ya zaman hakukuwa na Div6 na sasa zipo za kumwagaa..

watoto walipenda shule sahz wanapenda viduku na bongofleva
 
Zamani ndoa zinadumu hadi kifo...siku hizi unaoa leo jumatatu ikifika Ijumaa mshaachana

Zina andaliwa mazingira ya kutovumiliana kabla ya ndoa. Binti anataka awe na nyumba yake kabla. Ili likitokea lolote akimbilie uko.
 
Elimu ya zaman hakukuwa na Div6 na sasa zipo za kumwagaa..

watoto walipenda shule sahz wanapenda viduku na bongofleva

Bwahahahahaaaa..... div6 !!! Htr sana hii. Mi sipendagi, itokee tuu
 
watoto walikua na heshima lakini sasa hawana bahadhi wana watukana mpaka wazazi wao!

Kweli mkuu. Dogo m1 wa kike alikuwa form3 shule fln ya kata. Akachelewa wiki moja kwa kukosa ada! Akamwambia babaye "unadhani nimemkosa wa kunilipia iyo ela?!, nawaheshimu tuu!!" Dah, faza mtu hoi. Dogo alipata div 5 km sijasahau
 
Zamani bikra ilikuwa kitu cha kawaida zipo nyingi siku hizi bikra zimepotea kama pakti ya sukari baharini
 
Zamani wanaume walikuwa wakihudumia familia zao bila mchango wa wake zao. Lkn sasa wanatafuta wanawake wenye kazi ili wapige pasu ktk kutoa matumizi ya familia.
 
Zamani wanaume walikuwa wakihudumia familia zao bila mchango wa wake zao. Lkn sasa wanatafuta wanawake wenye kazi ili wapige pasu ktk kutoa matumizi ya familia.

Haki sawa ndio imefanya nyie muwe hivi
 
Zamani wanaume walikuwa wakihudumia familia zao bila mchango wa wake zao. Lkn sasa wanatafuta wanawake wenye kazi ili wapige pasu ktk kutoa matumizi ya familia.

Update me madam, ila nadhani zamani mwanaume alikuwa anaoa wake wengi na anakuwa na watoto wengi, yeye kazi yake ilikuwa kuwagawia mashamba then anakaa kitako kusubiri wake zake wamlishe na kila mke kutunza watoto wake, according to me siku hizi wanaume wamekuwa more responsible, isipokuwa watoto wa mama wachache wanaofugwa, which is an insult to my manhood.
 
Hii pilipili inawasha sana. Hawezi itumia uyu dada....
 
Back
Top Bottom