sakapal
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,804
- 1,425
Habari zenu wanajamvi wote na hongereni kwa kuingia 2013, amani na upendo kwenu wote. Jamani leo naombeni mnisaidie nimjibuje huyu binamu yangu maana tangu juzi ananipigia simu hajui afanyaje story ilianza hivi miaka kadhaa iliyopita.................
Hii ilimkuta binamu yangu kabisa ni kweli wala si story, (kosa kubwa wanalofanya wanaume wanaonyimwa watoto na wanawake waliozaa nao ni kutokuwa wawazi tangu mimba ina)poshika hadi mtoto kuzaliwa. Unajua nn, huyo binamu yangu alikuwa na boyfriend wake alikuwa anafanya kazi wakati huo binamu yangu yuko chuo, kufika mwaka wa pili binamu mimba ikashika huku na huku yule kaka akasema zaa chuo ntamalizia kukulipia kwani binamu alikuwa anasomeshwa na wazazi wake na mtoto ntalea si ninafanya kazi? binamu machale yakacheza akambembeleza jamaa akaitoa. Ile anamaliza mwaka wa tatu tu kabla hata ya majibu kutoka mimba ikakubali tena this time binamu hakuhofu kitu akijua sasa na harusi itafungwa kumbe jamaa alikuwa part time- hakuwa wa kuoa, ile kumwambia mimba imenasa jamaa akawaka mimba lazima itolewe na akampa na hela wakati ule alipewa Tsh 30,000/- gharama ya kutolea mimba (imeshapita miaka mingi tuu na mtoto now ni mkubwa) binamu huku na huku kachanganyikiwa akagoma kutoa ile mimba ila pesa alichukua ndo akanifata kwa ushauri je atoe mimba? na hela kanionesha huku akijiuliza kwanini niitoe hii mimba kama chuo nshamaliza na mie huyu jamaa nampenda na kama alikuwa hanipendi au hana mpango wa kunioa mbona iliposhika mimba ya kwanza alitaka nizae na huku akiniahidi atamalizia kunisomesha chuo kama nyumbani wangechukia mie kushika mimba wakati niko chuo? huku analia machozi nikamuonea huruma. Kwa akili yangu ya wakati ule nilimpa ujasiri na kumfariji kuwa asikate tamaa na asiitoe mimba as two wrongs does not make one right yaani kosa la kushika mimba nje ya ndoa na afanye na kosa la pili la kuitoa, nikamwambia je ukiwa unaitoa mimba ikagoma kutoka na ukajikuta unazaa mtoto mlemavu, je ukitoa mimba kikatoka na kizazi ukaja olewa aidha na yeye au na mwingine then watafuta mtoto wee utavumilia uchungu wa kutokuzaa hali ulitoa mimba kisa mwanaume haitaki? je kama huyu aliyetumboni kwako ni blessing from God utazuia mpango wa mungu? (kutokana na imani yangu) nikamwambia wajua hata yesu kabla ya kuzaliwa alikumbana na vikwazo vingi lakini kwasababu ilikuwa kusudi la mungu alizaliwa japo kwa shida nikamwambia tulia zaa mtoto wako jamaa atajirudi tuu na mtalea mtoto wenu na ile elf 30 nikamsindikiza akanunua cheni ya gold ya hela hiyo hiyo. Tena nikamwambia itakuwa ukumbusho wako kila uvaapo cheni hiyo juu ya mtoto utakayezaa. Basi home ikawa soo jamaa akakata mawasiliano kabisa thenk God akajifungua salama mtoto wake mzima mwenye afya tele. Baadae binamu yangu alipata kazi akamlea mtoto wake mwenyewe na mwaka mmoja baadae alimtafuta baba wake ili mauulize kwa mara ingine kama atajirudi yuko tayari kumsamehe ili wmlee mtoto wao pamoja. Jamaa akasema hana uhakika kama atamuoa na hataki kumuahidi chochote. Binamu yangu huku na huku miaka miwili baadae akapata mchumba aliyempenda kwa dhati na kuolewa huku huyu mchumba mpya akimlea mtoto wa binamu yangu kama wake na jina alimbadilisha liwe la ubini wa mumewe.
Sasa kuanzia siku baada ya xmas binamu yangu akanipigia simu anashida, yule baba wa mtoto wake amejirudi eti anataka mtoto wake amlee ameona na yuko na mke mwingine na anataka amsomeshe na kumtengenezea kadi ya matibabu, wakati huku yeye (binamu) na mumewe wanamlea kwa hali nzuri wala hajajua hata kama yule si baba yake halali. Jamaa anamwambia namtaka mtoto wangu binamu kachanganyikiwa kwani hataki mtoto wake aende kulelewa na mwanamke mwingine na bado hajamwambia mumewe mie bado sijamwambia cha kufanya ila naomba wanajamvi mnisaidie nimshaurije? mtoto mwenyewe anaumri wa miaka 10. Ushauri tafadhali.