Ndoa hizi!

Ndoa hizi!

DIKACY

Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
23
Reaction score
7
Mimi ni mkristu,nilifunga ndoa kanisani,nilipokua na ujauzito Wa motto Wa kwanza Mme wangu akapata mchepuko,baada ya mchepuko kusikia nimejifungua nayeye akabeba mimba,Mme wangu akawa amechanganyikiwa aishi name yupi kwa maana alisema hawezi kua na wake 2,Akaamua kuokoka ili Mungu amuonyeshe nani mke wake inawezekana alifanya makosa kuoa mke Wa kwanza,akaenda Malawi kwa Prophet bushiri akatabiriwa aache mke Wa ndoa aoe mchepuko,alivyorudi akaongoza mahakamani kwa ajili ya talaka,talaka imeshatoka kwa maana mke wake hakutaka kelele nae,tatizo lililopo,hataki hata kujiua mtoto wake anaendeleaje,matumizi mpaka mpigizane kelele,inauma sana mtoto kukosa mapenzi ya baba,ushauri tafadhari.
 
Ushauri fanya mambo yako wala usimfikirie huyo poyoyo, kuhusu matumizi ya mtoto sheria zipo wazi akisumbua mshtaki ustawi wa jamii hilo halina mjadala, ila jaribu kumpoteza kwenye fikra zako ingawa kiuhalisia inauma sana, na pia nikupe pole sana, ni mitihani tu ya kidunia huwezi jua labda ni mpango wa Mungu umeepushwa na jambo baya/mabaya bwana huyu angekufanyia. Mwisho wa siku utampata mtu sahihi na anaejielewa.
 
Piga moyo kononde dada maisha yasonge, unajua katika maisha haya nilijifunza anaweza asikufae kabisa ndugu wa damu akajakukufaa mtu baki wa mbali kabisa tena wala hauna undugu nae na wala si damu yako
 
Ikiwa una uwezo wa kumlea bila msaada wake fanya hivyo kama huna basi rudi pale ilipopewa talaka najua yapo masharti kuhusu mtoto
 
Huko mahakamani walikowaachanisha hawakutoa muongozo wa huduma kwa mtoto?

Usimlazimishe mamy,lea mwanao na hivi ni mmoja tu hatokushinda ulezi.

Kuhusu mapenzi ya Baba pia yasikuumize kichwa,waangalie yatima na wajane wanapata upendo wa kutosha kutoka kwa aliye mume wa wajane na Baba wa yatima,hatokuacha nawe na mtoto Wako msiache kumtumainia.
Likuepukalo una heri nalo.
 
Mimi ni mkristu,nilifunga ndoa kanisani,nilipokua na ujauzito Wa motto Wa kwanza Mme wangu akapata mchepuko,baada ya mchepuko kusikia nimejifungua nayeye akabeba mimba,Mme wangu akawa amechanganyikiwa aishi name yupi kwa maana alisema hawezi kua na wake 2,Akaamua kuokoka ili Mungu amuonyeshe nani mke wake inawezekana alifanya makosa kuoa mke Wa kwanza,akaenda Malawi kwa Prophet bushiri akatabiriwa aache mke Wa ndoa aoe mchepuko,alivyorudi akaongoza mahakamani kwa ajili ya talaka,talaka imeshatoka kwa maana mke wake hakutaka kelele nae,tatizo lililopo,hataki hata kujiua mtoto wake anaendeleaje,matumizi mpaka mpigizane kelele,inauma sana mtoto kukosa mapenzi ya baba,ushauri tafadhari.

Hii story ni wewe au umehadithiwa?
Mwanzo ulivaa uhusika,mwishoni ukamvika mtu mwingine...
Anyway
 
Hii story ni wewe au umehadithiwa?
Mwanzo ulivaa uhusika,mwishoni ukamvika mtu mwingine...
Anyway

mkuu kumbe na wewe umeliona hilo!! ajipange kwanza.....
 
Swali, wewe umeokoka?

Aisee huo utabiri mi nauona feki. Mungu hawezi kukuamru umuache mke wa ujana wako hata kama mlikosea.

Kama umeokoka, tulia kwa Mungu umuombe ili Mungu amrejeze mumeo mlee mtoto.

Kama hujaokoka pia nakushauri kama unauwezo wa kulea achana nae. Hiyo ndoa alioao haina mda mrefu. Kesho au kesho kutwa auhakika asilimia 90 atarudi kwako kwa magoti kyomba umsamehe.

Pole sana dada
 
Hawa watu wanaojiita ma Prophet hao siwaamini hata kidogo .

Tafuta Kazi tunza mtoto wako. Achana na mwanaume ambaye amekuacha .
 
Back
Top Bottom