Ndo nini interview kuweka siku moja?

Bravo H

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2014
Posts
221
Reaction score
88
Hawa utumishi wangeweka ratiba tofauti ya interview sababu siku moja kuna interview ya nssf, magereza, TAA, na wakala wa vipimo, na wafanyaji wa interview ni watu wale wale wanajirudia, ushauri siku nyingine mpeane mda.
 
Hizi ni mamlaka tofauti zinazojitegemea kiutendaji. Kwa hayo wasailiwa wanatakiwa "wajiongeze" wengewe.
Kila la kheri wasailiwa wa hizo interviews za 13/12/2014..
 
Umesahau na bodi ya utalii nao wameita watu kwa ajili ya usaili wa kuandika trh hiyo hiyo mkuu.
Sasa ni shidaaaaaaaaaa..
 
Kama mtu umeitwa sehemu zote zilizoita interview bora usiende maana tayari una mkosi mpaka hapo.
 
Wamefanya jambo la heri kuzuia mrundkano usiyo wa lazma

yan nssf tra bod ya utalii utumish zote upate ww wengne wakose
 
Mimi karata yangu imedondokea NSSF,utumishi na TTB watanisamehe kwa kweli..
 
Hawa utumishi wangeweka ratiba tofauti ya interview sababu siku moja kuna interview ya nssf, magereza, TAA, na wakala wa vipimo, na wafanyaji wa interview ni watu wale wale wanajirudia, ushauri siku nyingine mpeane mda.

Hizo taasisi zote hazikupitishia utumishi?
 
Mi nimeitwa wakala wa vipimo kwa post mbili tofauti muda na siku moja....majanga!😕
 
Taasisi tofauti na wanafanya maamuzi tofauti.. hiyo ni coincidence kwako tu wala si kwao.. Sio kila jambo la kulalamika.. cha msingi ni kufanya maamuzi..
 
jamani hivi nssf wanakubali transcript tu bila mambo haya ya vyeti?
 
Yani mnataka mpate kote, nyie ndo mnanyima kazi wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…