Ndiyo maana Fernandez kaenda kuwekeza NALA Kenya

je parle

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,883
3,621
Tanzania ni nchi isiyotaka kuenda sawa na Dunia ya kileo. Bado uswahili mwingi mno ,

Niende kwenye mada. Leo nilitumiwa kihela kidogo tu kutoka huko nchi za wenzetu, basi nikaenda bank ya karibu yangu kutoa kupitia moneygram, doh salaleeeeeee

Nimepigwa maswali kama ya DP World wakati Hela yenyewe hata Milion 1 haifiki. Sasa Mimi nikaanza kujibishana na teller badala ya kumjibu kiufasaha kwa sababu imeniuma kuona Hela ndogo alafu maswali ni mengi KULIKO Hela yenyewe

Eti wanataka Hadi supporting documents kwnn umetumiwa hiyo Hela. Nimechoka choke Yan kahela haka ndio maswali chungu mzima ATI aliekutumia unafajamiana nae tangia muda gani?

Yaani maswali ni mengi siwezi kuya andika hpa naona kama pages za jamiiforums hazitoshi. Ndio maana yule bwana alienda kufunguka ofisi Kenya mana hapa tz ni upuuzi kwa kwenda mbele

Badala waruhusu Hela ziingie zaidi kutoka abroad wao ndio kwanza wanatengeneza vikwazo au wanapenda hela ziwe zinaenda tu nje ya nchi kununua bidhaaaa?
Wanaogopa Nini haswa?

Ndio sheria mpya au Kuna nini
 
Nchi yetu inapenda kubinya watu wasio na hatia, ila wanaopitisha izo pesa za kufadhili vikundi vichafu wala hawana habari nao.
Kuna kipindi nmeenda benki ya DTB kutoa kitita kutoka USA via WORLD REMIT wanakuangalia kama gaidi maswali kibao .... thanks nowadays mzgo unaingia kwa m pesa tuu....
 
Standard charter babyeeeeeeeeeeeess
Benki kubwa achana na microfinance
IMG_0250.jpg
 
Maccm huwa, yanalala, mimacho kodo, yanaogopa kupinduliwa, ndio yanatunga Sera za, fedha za, hovyo kuzuia wapinzani wao, wasipate msaada, kutoka nje, yanahofia sana wananchi wakiwezeshwa kiuchumi na fedha za diaspora, yana kuwa, na, Amani, pale wananchi wanapokuwa, maskini
 
Back
Top Bottom