ndege ya Precision yapata ajali Kigoma.

Heri Mungu amewanusuru na balaa...Nimepanda ndege ya Presicion Mwanza-Kia leo..Tairi mbili za nyuma zilikuwa vipara kinoma mpaka nyuzi za tairi zinaonekana...Niliposoma hii habari nikakumbuka hizo tairi kweli zinaogofya....bei isiseme nimenunu return ticket kwa 450,000/= sijui nakwenda Dubai au???????hii ni tkt valid for three months
 
ajali ya aina hii inatokana na makosa ya rubani wakati wa touch down, hasa akiwa mwanafunzi.
 
Nasikia Lukuvi ameamrisha ikimbiziwe mahakamani ili kutuziba midomo isiongelewe nje ya mahakama!

Hahahahaaa wewe mkuu kiboko sana, nimecheka mpaka kuilike hii
 
Niko Kigoma toka DSM lakini nimegundua hawa marurubani wana maneno/tararira na majidai sana ya maneno kushinda marubani wengine duniani, Maneno mengiX2 sana wawepo angani, Nilishangaa.too much pomps kenye mike.
 
Tz kama Nollywood,kila siku tunaachia filamu mpya........Lord have mercy!
 
Mola atuepushie janga. Precision jamani kagueni vizuri ndege hizo.
 

Rushwa ikisha shamiri kutokana na udhaifu wa watawala basi ajali,maafa na matukio mengi ya kizembe inakua jambo la kawaida!
 
Rubani wa ile Ndege alipiga hesabu mbovu wakati anatua almost alitua kuanzia katikati ya uwanja na huo uwanja hivi sasa uko kwenye matengenezo akagundua run way inakwisha ndege bado iko speed akalazimika kukamua breki kali ndizo zilizopelekea kupasua tairi 3 nyuma otherwise huenda ingekuwa ni hatari zaidi. Kwani mwishoni mwa uwanja ndimo jamaa wanatengeneza na wameweka magreda na malori yao....Noumi
 

mkuu naomba kutofautiana nawe. ukitoka Dar kwenda Entebbe unatua KIA then unaendelea moja kwa moja hadi Entebbe na ukitoka Entebbe unatua KIA na kisha moja kwa moja hadi Dar. Hiyo ya kuzunguka miji yote ya Afrika mashariki, umeongeza chumvi isiyo lazima. ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…