Ndege kubwa zaidi zilizowahi kuundwa duniani

amygdala

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,082
997
Tangu binadamu alipofanikiwa kuunda ndege na kupaa angani, wataalamu wamekuwa wakijitahidi kuunda ndege kubwa na kubwa zaidi.

Wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, majaribio ya kwanza ya kuunda ndege kubwa zaidi yalifanyika.

Ndege hizo zilikuwa na injini kadha, na zilikuwa na uwezo wa kubeba na kuangusha mabomu mengi.

Kabla ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kuliundwa ndege kama vile Dornier Do X ambayo ilikuwa kama meli kubwa na ndege ya ANT-20 ya Muungano wa Usovieti ambayo ilikuwa kubwa ajabu.

ANT-20 ilikuwa na uzani wa tani 50 ilipokuwa inapaa, na mabawa yake yalikuwa na urefu wa futi 207 (mita 63). Ndege hii ilikuwa na chumba chake cha kupigia chapa, ukumbi wa sinema na chumba cha kutolea picha.
Kuundwa kwa injini ya jeti kuliwezesha ndege kubwa na nzito zaidi kuundwa.

Ni hapo ambapo ndege kubwa kama vile Airbus A380, ndege ya ghorofa yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 850 ziliundwa.

Kuliundwa pia Antonov An-225, ndege kubwa ya mizigo ambayo inaweza kubeba mizigo ya tani 250. Ndege hiyo ni kubwa kuliko ambali ambao ndege ya kwanza ya Ndugu ya Wright ilisafiri mara ya kwanza ilipofanikiwa kupaa.

Hapa chini ni mkusanyiko wa baadhi ya ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa.

(Picha ya Convair B-36 imetoka kwa Clemens Vasters katika Flickr).

_96194488_3d45cca5-37e4-48a1-849c-592037f6a9d8.jpg
Haki miliki ya pichaSAN DIEGO AIR AND SPACE MUSEUM
Image captionNdege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia ilikuwa Zeppelin-Staaken R.VI, ndege ambayo ilizifanya ndege za wakati huo zionekane kama mifano tu ya ndege. (Picha: San Diego Air and Space Museum)
_96194489_bc5f2434-a485-4ce0-96fc-ac831c1ec289.jpg
Haki miliki ya pichaBUNDESARCHIV
Image captionNdege nyingine kubwa kutoka Ujerumani ilikuwa Dornier Do X, ilifanana na meli na ilikuwa injini 12. Iliweza kubeba abiria hadi 100. Ilikuwa na uzani wa tani 56. (Picha: Bundesarchiv)
_96194490_9001a01a-f14c-4d9b-b2e2-e053705e478c.jpg
Haki miliki ya pichaWIKIMEDIA COMMONS
Image captionANT-20 iliyoundwa na Tupolev ilitumiwa kama chombo cha propaganda, ilikuwa na kituo cha redio, ukumbi wa sinema na chumba cha kutoleshea picha. Ilikuwa na injini kubwa juu ya mgongo wa ndege kuiwezesha kupaa. (Picha: Wikimedia Commons)
_96194491_bcf41123-829d-415d-9c9b-bdca4e556396.jpg
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ilikuwa B-29 iliyoundwa na Boeing. Ndiyo iliyoangusha mabomu ya atomiki Japan. Ilifungua ukurasa mpya wa ndege za kuangusha mabomu za kusafiri masafa marefu. (Picha: Getty Images)
_96194492_cd1e24b4-7f07-404b-8c06-53b5e531c3cd.jpg
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionH-4 Hercules iliyoundwa na Howard Hughes ina mabawa marefu zaidi duniani kuliko ndege nyingine yoyote. Hata hivyo ilipaa angani mara chache tu. (Picha: Getty Images)
_96198032_01043c9c-70f3-4513-b59a-305e1383020c.jpg
Haki miliki ya pichaCLEMENS VASTER
Image captionConvair B-36 Peacemaker ilikuwa ndege ya kwanza duniani ya kuangusha mabomu kuweza kusafiri kutoka bara moja hadi bara jingine. Ilitumiwa injini kadha za jeti na rafadha kadha kuweza kupaa. (Picha: Clemens Vaster)
_96198033_44ffec52-76fe-4eb6-83da-10532aaf13ec.jpg
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionB-52 Stratofortress iliyoundwa na Boeing inasalia kuwa moja ya ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani. Ilitumia injini nane kubwa. (Picha: Getty Images)
_96198034_68355c3f-7797-4ddf-b721-fca5a5bc02ec.jpg
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTu-160 ya Tupolev ingeweza kubeba jumla ya tani 275 ikipaa, na ilikuwa na mabawa makubwa zaidi yaliyoweza kujipinda kuwahi kuundwa. (Picha: Getty Images)
_96198035_0a478558-30e0-4819-9097-beea100800db.jpg
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIngawa Boeing 747 ilikuwa ndege ya kwanza kuitwa Jumbo Jet, A380 ya Airbus ni kubwa kuliko Boeing 747. Ndege hii inaweza kuwabeba watu 850. (Picha: Getty Images)
_96198036_ba093c5f-b69b-4669-a78c-843d4f69bb8b.jpg
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani ni An-225 ya Antonov ambayo ina injini sita na urefu wake ni mita 84. Ndege hii ina uwezo wa kubeba karibu tani 250. (Picha: Getty Image
Ndege kubwa zaidi zilizowahi kuundwa duniani - BBC Swahili
 
Ma professor na ma engineers wanaweza kuambia madini yanayo tumika kutengeneza engine za hayo mandege wapo vizuri sana haswa professor aka muhongo
 
Back
Top Bottom