Unanikumbusha mbaali sana, enzi flani nikiwa Mgulani j... Jioni wakati wa kurudi, magari ya mbagala yalikuwa ya shida sana, yaani wakati wa kupanda mnagombania na unaweza kuingizwa ndani kwa kubebwa juu juu, mtajikuta midume mitupu
Dah! hawa huwa wanakera mno, na miongoni mwao ni makondakta wenyewe anafanya kazi kutwa nzima na nguo iliyokatwa mikono, basi akipita kukusanya pesa kwenye gari iliyojaa ni raha tupu
Daladala kiboko!
Ukute umevaa smart mkanda nje na kiatu umepiga kiwi ukishuka unaweza sema umebadilishiwa viatu miguuni sio vumbi ni hatari !
Joto sasa miaka michache ya nyuma kulikuwa kuna daladala zimaanzia kariakoo to Mlandizi hizo zilikuwa ni kupitia madirishani tu na lazima ngumi zichapwe kugombea siti we fanya mchezo mwenzako kazama dirishani alafu kaingia eti umeweka kimfuko chako kwenye siti kuonyesha ina mtu alafu anakuja anaondoa mzigo anakaa balaa lake asikuambie mtu visu sikumoja vilitolewa kisa siti
Umevaa kibrazamen Tshirt na jeans enzi hizo za kila mmoja anapendeza chini raba nyeupeee unataka gari za kariako -ubungo via Tandale uzuri ukifika raba kama umetoka shambani hahaaa.
nakumbuka kipindi nimepiga iyo kazi
hako kamchezo siku ya siku
mshikaji kabugi kwa mjeshi wa jkt
wokovu kacheza na msambwanda
hadi kamchafua kufika jkt ya kwanz
a kushuka si kashuka na jamaa sijui kama atakuja kusahau kilichompata#