Mtuflani Official
JF-Expert Member
- Dec 31, 2019
- 1,950
- 4,390
Nchi yetu miaka michache ijayo tutaanza kupambana na Wachina. Inakuaje mchina anakuja nchini kufungua supermarket. Wachina wametapakaa kila kona ya hii nchi wanachukua fursa za Watanzania. Juzi bungeni mbunge wa Geita vijijini alitoa tahadhari kuhusu Wachina kupewa migodi wakati wana mitaji ambayo Watanzania wanaweza kuwa nayo. Nilisikitishwa sana na jibu la Mh Spika akidai kwamba mambo mengine ni kulinda diplomasia. Yaani mtu aje nchini kwako kuchukua fursa za wazawa wewe usite kuchukua hatua eti kisa diplomasia. Hii sio sahihi.
Pili kwanini tusirudishe sera ya Magufuli. Hakuna kuruhusu kampuni yeyote kuajiri zaidi ya raia wa 5 wakigeni. Hii itasaidia kujenga uwezo kwa raia wa Kitanzania. Magufuli aliweka kikomo kwenye vibali kwa raia wa Kigeni ili kuwezesha kujengewa uwezo. Hakuna kazi yeyote hapa nchini inashindwa kufanywa na wazawa . Imenichukua muda kuelewa kwanini Magufuli alichukua hii hatua. Hawa watu wanaipiga sana serikali kwa kupunguza makadirio ya mapato kwa sababu kuwaruhusu kwa wingi kwenye makampuni kunawawezesha kutengeneza mtandao wao vizuri. Ushahidi upo.
“Tusipoimarisha uwezo wa watu wetu kushiriki katika uchumi, tutajikuta tunagawana umaskini baadala ya kugawana utajiri. Ni kwa sababu watu wetu hawana ujuzi na elimu ndo maana tunapata wawekezaji uchwara ambao wanakuja kuchukua fursa za Watanzania……” Rostam Aziz