Nchi inafanya nini kuwaandaa vijana kuja kuwa viongozi wajao?

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Kitu ambacho kimewahi kunishangaza ni kusikia Salim Ahmed Salim alikuwa balozi akiwa na miaka 25. Kipaji chake kilionwa na Karume na akampendekeza kwa JK Nyerere (Naruhusu kukosolewa).

Kazi kubwa ya kiongozi ni kumuandaa wa chini yake kuja kuwa kiongozi bora tena ikibidi zaidi yake. Mfano Mao Alimuandaa Deng Xioping na vijana wengine waliokuja na ideas za market economy China tunaiona leo. Vijana hawa wakiwa wadogo walikuwa Ulaya na Urusi wakijifunza mambo kwa ajili ya nchi yao na kuja kuwa viongozi wa baadae. Lee Kuan Yew (Singapore) aliagiza graduates waoane ili nchi iwe na Elite Society itakayowasaidia wengine wengi kutatua matatizo yao. Alexander The great (20's) alitawala dunia lakini baba yake alimpeleka akaishi kwa philosopher Aristotle kufundwa uongozi akiwa mdogo hadi alipofikisha miaka 16.

JPM anaonekana anatamani kutumia vijana kutimiza ndoto yake Tanzania. Unadhani kuna vijana wa kutosha Taifa limewaandaa kuja kuwa viongozi wa taifa hili na kulivyusha kwa mkono wa chuma? Je kwa sasa Taifa linatambua umuhimu mkubwa wa kuwaandaa vijana wake? Hawa wachache tunaowaona ni mazao ya bidii zao au leadership progressive plan ya taifa?

Unadhani nini kifanyike na kwa vipi hawa wazee wetu wanapoondoka Taifa liwe na bwawa kubwa la akiba ya vijana watakao simamia rasilimali zetu zinazotamaniwa na kila taifa.

Najaribu kuwaza!
 
Mkuu
Kitu ambacho kimewahi kunishangaza ni Kusikia Salim Ahmed Salim alikuwa Barozi akiwa na miaka 25. Kipaji chake kilionwa na Karume na akampendekeza kwa JK Nyerere(Naruhusu kukosolewa).

Kazi kubwa ya Kiongozi ni Kumuandaa wa Chini yake kuja kuwa kiongozi bora tena ikibidi zaidi yake. Mfano Mao Alimuandaa Deng Xioping na vijana wengine waliokuja na Ideas za Market economy China tunaiona leo. Vijana hawa wakiwa wadogo walikuwa ulaya na urusi wakijifunza mambo kwa ajili ya nchi yao na kuja kuwa viongozi wa baadae. Lee Kuan Yew (Singapole) aliagiza graduates waoane ili nchi iwe na Elite Society itakayowasaidia wengine wengi kutatua matatizo yao. Alexander The great (20's) alitawala dunia lakini baba yake alimpeleka akaishi kwa philosopher Aristotle Kufundwa uongozi akiwa mdogo hadi alipofikisha miaka 16.

JPM anaonekana anatamani Kutumia Vijana kutimiza ndoto yake Tanzania. Unadhani kuna vijana wa kutosha Taifa Limewaandaa Kuja kuwa viongozi wa taifa hili na kulivyusha kwa mkono wa chuma? Je kwa sasa Taifa Linatambua Umuhimu Mkubwa wa kuwaandaa vijana wake? Hawa wachache tunaowaona ni mazao ya bidii zao au leadership progressive plan ya taifa?

Unadhani nini kifanyike na kwa vipi Hawa wazee wetu wanapoondoka taifa liwe na Bwawa Kubwa la akiba ya vijana watakao simamia rasilimali zetu zinazotamaniwa na kila taifa.

Najaribu kuwaza!!!

Tatizo ninalo liona kwa jamii yetu ni kwamba hatuna utaratibu huo wa kuandaa vijana. Kwanza wazee wenzngu wanisamehe. Wazee wa Taifa letu wamejawa ubinafsi ndo maana unaona hata wengi wanapofikia muda wao wa kutumika (kustaafu), wanaomba waongezewe muda wa kuendelea kufanyakazi kwa madai kuwa wao tu ndo wenye uwezo wa kuendesha aidha shirika au taasisi. Tatizo jingine ni kwamba viongozi wetu walio wengi siyo waadilifu, na mara nyingi nafasi zao wanapostaafu wanapendekeza watu waliokuwa wakishirikiana nao kufisadi. Aidha kwa malengo ya kuwapa ulaji watu wao au kulinda madhambi waliyofanya yasije yakafichuliwa na mtu mwingine. Hata kama Bwana Mkubwa anataka kuwatumia vijana kwenye serikali yake, bado mimi naona ufanisi unaweza kuwa kidogo kwa sababu sifuatazo. Kwanza hawa vijana hawajaandaliwa kuwa viongozi. Pili kutokana na mfumo wa ufanyaji kazi na maisha kwa ujumla nchini kwetu, hawa vijana wengi wana nidhamu ya woga (hapa namaanisha ni pretenders). Kwa sababu hawa vijana tunawaona hawana subira. Wengi wao wanapotoka chuo akipata kazi ndani ya mwaka mmoja au miwili waishi maisha ya ndoto zao. Hivyo wakipata nafasi ya kupiga deal kama wanavyosema wanapiga sana. Ila ninachokiona kwa sasa ni kwamba vijana wanapretend kuwa waadilifu kwa sababu baba hataki upuuzi. Lakini mawazoni mwao hawako hivyo. Pindi Bwana Mkubwa akiondoka, hawa vijana wanaweza kuonyesha their true colors. Kwa hiyo Mimi ningeshauri Bwana Mkubwa japokuwa ana nia nzuri kwa vijana, bado anapaswa kuwa mwangalifu sana.
 
Wazee wameng'ang'ania nafasi si kwa kupenda bali kwasababu ya pension scheme mbovu...tukirekebisha hapo wote wataachia ngazi...vijana nao wamebaki kujipendekeza na kushindwa kutumia ujuzi na nguvu zao kulitumikia taifa kwakuwa ajira hazitengenezwi kwakua wazee wengi wako busy na kutengeneza projects zisizo na tija ili kujipa pension baadaye.....kiujumla tatizo kubwa lipo kwa unertainty iliyopo kwenye life after office...every body is trying hard to have life insurance after office ndiyo maana every where throughout the contry corruption is an order of day..
 
uko sahihi, nini kifanyike?
 
Unamaanisha tukiwa na stable na reliable pension schemes, na kuwapa wazee uhakika wa maisha baada ya kustaafu tunaweza kuwafanya wakaanza kufikiri nyuma na kukumbua jukumu la kunurture vijana. Lakin Dunia ya sasa inaendeshwa na wajasiliamali makini. Huku vijana hawawezi kuwa developed katika Leadership and management huku wamejikita katika Start up and entrepreneurial projects wakati bado hatujawa na sustainable pension schemes. Hapo vipi cheif
 
Kuwa na stable pension scheme au social support ni jambo la mhimu sana, hasa ukiendana na vijana kuandaliwa. Kwanza wazee hawatakuwa na hofu ya kustaafu. Kitu kingine ambacho mimi nakiona ni tatizo kwa jamii yetu ni kwamba watumishi wengi, siyo tu serikalini bali hata sector binafsi hatujui kazi tunazozifanya ni za kwetu, yaani tunachukulia tu kwamba unamfanyia boss. Lakini jamii ingeelimishwa, tokea kuanzia ngazi ya familia, mashuleni, hata vyuoni, kusingekuwa na utendaji mbovu kama tunaoushuhudia hapa kwetu. Nasema hivi kwa sababu zifuatazo; Jamii kama ingeelimishwa na kujua kuwa mtu anapoajiriwa hiyo kazi ni ya kwake hamfanyii mtu mwingine ni Kwa manufaa yake, kizazi chake na taifa kwa ujumla, basi wizi na ubadhilifu wa mali ya umma ungepungua kwa kiwango kikubwa. Leo hii hapa kwetu, mimi naweza kuwa mtumishi wa chini, najua jinsi boss wangu anavyofanya ubadhirifu. Lakini nashindwa kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika. Au watati mwingine natoa taarifa hizo za ubadhirifu kwa mamlaka husika lakini kwa vile jamii nzima imeoza kwa rushwa nakuwa kama nimewapa ulaji wale wanapaswa kudhibiti ubadhirifu. Badala ya mbadhirifu kuchukuliwa hatua, badala yake wasimamizi niliowapa taarifa wanashirikiana na muharifu kuendeleza ubadhirifu.

Kuna wakati huwa najiuliza nashindwa kupata jibu sahihi kama kweli jamii yetu tuko sawa. Mfano, imetokea mtumishi wa umma ofisini kwako amefanya ubadhilifu hachukuliwi hatua zozote. Pia anaendelea kusema mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake. Hii ina maana jamii yetu hatujali kizazi kijacho nacho kikute shirika lipo, nao wapate kazi maisha yaende. Tunajijali sisi tu. Hivyo, ili jambo hili lifanikiwe tunahitaji transformation ya mindset zetu.
 
Unamaanisha tukiwa na stable na reliable pension schemes, na kuwapa wazee uhakika wa maisha baada ya kustaafu tunaweza kuwafanya wakaanza kufikiri nyuma na kukumbua jukumu la kunurture vijana. Lakin Dunia ya sasa inaendeshwa na wajasiliamali makini. Huku vijana hawawezi kuwa developed katika Leadership and management huku wamejikita katika Start up and entrepreneurial projects wakati bado hatujawa na sustainable pension schemes. Hapo vipi cheif
Hii ni issue ya kuku na yai hakuna inayoweza kuanza kabla ya nyingine...we need big push ambayo tumepatiwa na Mh. Rais Magufuli whats now needed ni elites katika taakuma zao ku sacrifice na kuondoka katika comfort zones z
 
uko sawa
 
Back
Top Bottom