Nchi imepinda,inahitaji kunyooshwa.

ong'wafaza

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
262
Reaction score
115
Ndugu wana JF,
Kumekuwa na mtazamo kwamba nchi yetu imegubikwa na maovu mengi yakiwemo mambo ya ufisadi,biashara haramu na upigaji dili yakitamalaki miongoni wa wananchi na hata baadhi ya viongozi kwa muda wa miongo kadhaa.Na kwa mkutadha huu,nchi imepinda.
Mimi pia ni miongoni mwa wanaouona ukweli huu.
Kumekuwa na maoni mbalimbali miongoni mwa jamii kuhusu namna ya kujinasua na madhila haya kama nchi.
Baadhi ya wananchi wamekuwa wanapendekeza kuwa zitungwe sheria kali zitakazoweza kusaidia kuinyoosha nchi ikiwemo kubadili katiba ya nchi.
Wengine wamekwenda mbali zaidi wakisema kuwa pale nchi hii ilipofikia,na ili iweze kunyooshwa,panahitajika tupate kiongozi dictator .
Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa sisi wanajamvi kutoa mchango wetu kupitia uzi huu ili tusaidie tumsaidie Mheshimiwa rais wetu katika jitahada za kuinyoosha nchi badala ya kubeza juhudi zake
Si vyema pia kwa sisi kama Wadau wa Serikali kukaa kimya bila kuchangia lolote.
Binafsi napendekeza tuanze na kutengeneza katiba ya nchi itakayokidhi na kutanzua matatizo yaliyotufikisha hapa kama nchi.
Kwa kuzingatia hili, uhuru wa kutoa maoni na kujieleza uwe mpana zaidi ili mradi sheria,kanuni na taratibu zetu tulizojiwekea zifuatwe.
Je,wewe una maoni gani?
Karibuni tuchangie kwa staha tusaidie kuinyoosha na hatimaye kuijenga nchi yetu.
Nawasilisha.
 
Nadhani ni nia ya dhati kabisa ya mh. Rais wa awamu hii kuinyoosha nchi hii baada ya kupinda kwa muda mrefu tangu awamu ya kwanza pale wapindaji walipomzidi nguvu mwalimu Nyerere na kumuua Karume na Sokoine.

Kwa sasa Mh. Rais amekuja na kuanza na njia nzuri sana ya kuinyosha nchi.
Kwanza ameanza kuwatoa wafanyakazi hewa.
Pili akawatoa wenye vyeti hewa. Hawa walikua ndio wanaotumika kupindisha nchi.
Tatu amewabana wafanyabiashara haramu waliokua wanafadhili vyama vya siasa ikiwemo kuipatia CCM ushindi wa kununua huko majimboni .

Nne ameanza kukinyoosha chama chake cha CCM ambacho ni adui mkubwa wa maendeleo endelevu ya watanzania kwa kusimamia nidhamu wakati huu wa uchaguzi wa ndani.
Ikumbukwe kuwa CCM ndiyo iliyoua azimio la Arusha .
CCM ndyo iliyoleta ubepari uchwa na kuweka pembeni ujamaa.
CCM ndyo iliyokuja na sera mbovu za ubinafsishaji.

CCM ndiyo iliyovuruga mchakato wa katiba ya warioba.
CCM ndiyo inayoharibu uchaguzi wa Zanzibar kwa manufaa ya wachache kwa kuwadanganya wazanzibari kuwa wakichagua chama kingine Sultani atarudi kutawala.

Kwa hiyo ukitaka kuinyoosha nchi hii ni LAZIMA KWANZA UINYOOSHE CCM na matajiri wengi ambao ni wezi waliotokana na wizi wa kiCCM. Hawa ndio wanaokua tishio harakati za kimfumo na kimageuzi.

Pindo kubwa la nchi hii ni CCM na wafanyabiasahara haramu waliokua wanauza mpaka twiga na tembo hai nje ya nchi. Bila kusahau wale wafanyabiashara wa unga.

Mh. Rais ameanza vizuri pia kwa kumweka Polepole na Profesa Kabudi kwenye uongozi.

Baada ya kuwatoa wale wote wanaokwamisha zoezi la kuinyoosha nchi kimfumo ndipo sasa Mh. Mkuu wa nchi alete katiba ya Warioba ili ipitushwe upya.
Japo Kipengele cha serikali tatu ni pindo, kitolewe.
Serikali iwe moja au zibaki mbili na mengine yabaki kama yalivyo hasa kipengele cha maadili ya uongozi wa umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…