Nchi imegawanyika mapande mawili sakata la Bandari

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,302
Sasa ni wazi kuwa Sakata la Bandari limetugawanya MAPANDE MAWILI. Wapo wanaopinga mkataba tata na Wapo Wanaounga Mkono.

Sababu kubwa za kupinga ni pamoja na usiri, utata na Namna Mchakato mzima wa Ulivyofanyika wa Kumpata DP WORLD na Kesi za DP WORLD na Nchi mbalimbali katika Masuala ya Bandari.

Watanganyika Wanauliza
Kwanini Mkataba hauna Ukomo? Nani alimtafuta mwenzake ni DP WORLD au ni Serikali? Kama ni Serikali mbona tenda haikutangazwa kama Sheria inavyotaka? Kama ni DP WORLD kwanini alileta hili wazo ana uchungu gani na bandari yetu?

Kwanini Wafanyabiashara Wakubwa kina Rostam Aziz wanashabikia sana Bandari kuwekezwa wana maslahi gani? Kwanini wabunge, Waandishi wa Habari walipelekwa Dubai kwa suala hili mbona kwa Wawekezaji wengine hatusikii kwenda?

Kwanini wadau wa masuala ya bandari hawakupewa muda wa kutosha kutoa maoni na Mapendekezo yao?

Maswali ni mengi, yote hayo yanaleta utata wa mkataba huu. Kwanini wabunge wanatumia nguvu kubwa kuwatisha Watu wanaokosoa huu Mkataba?

Tunaambiwa DP WORLD ataongeza Mapato Wakati mapato ya bandari yanaibiwa na Watendaji wetu na Hakuna hatua zinazochukuliwa (Report ya CAG na PAC ya BUNGE).

Watanganyika tunataka bandari yetu huu ni Mkataba umeshamiri Usiri unaifichwa na Wahusika huwezi kuwa na Mkataba unaompa maslahi makubwa mpangaji kuliko mwenye Nyumba huwezi kuwa na mkataba usioeleza ukomo wake.
 
Mpaka sasa naona tupo salama, kadiri siku zinavyozidi kwenda nauona mshikamano mkubwa kwa makundi yote yenye nia njema na nchi hii kwenye sakata hili bandari kuanzia viongozi wa dini zote,wasomi ,viongozi wa upinzani, wananchi nk
 
Tangu lini wanawake wakawa na uchungu na mali aliyotafuta Baba wao kazi yao ni kutumia na kula bata.Kosa kubwa tumewapa wamama mihimili mikuu hili ni kosa na vita vikitokea watakaoumia zaidi ni Wanaume wa Tanganyika,wanaume amkeni amkeni naseama amkeni.Chelewa chelewa utakuta mwana si wako.
 
Uwiiiiii punguza makali ili tufike tuendako
 
Kwa ufupi naona ni kuamua tu kuhusu sakata hili kwamba wanaounga mkono sakata la DP world waende Zanzibar na tunaopinga sakata hili tubakie Tanganyika ili ubishi uishe simple.
 
Majaribio yote kutuondoa kwenye mjadala wa BANDARI yameshindikana.

Kuna kiongozi mmoja aliwahi Sema kuwa sisi Watanzania hatuna tunalolijua zaidi ya kuongea na kusahau.

Tutajua tu mwisho wake.
 
mama anaupiga mwingi
 
Mbona unaficha ukweli wenyewe kuwa ni CCM ndio msiba mkubwa hapa Tanganyika.
 
Wewe mwenyewe umelala mana huna unalofanya....
 
Mpaka sasa naona tupo salama, kadiri siku zinavyozidi kwenda nauona mshikamano mkubwa kwa makundi yote yenye nia njema na nchi hii kwenye sakata hili bandari kuanzia viongozi wa dini zote,wasomi ,viongozi wa upinzani, wananchi nk
Hata wale tuliowapa dhamana wenye tabia ya unyumbu wameanza kutoahirisha kufikiri
 
Watanzania kwenye hili wamegawanyika zaidi ya mapande mawili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…