NCCR yamfukuza uanachama Kafulila na wenzake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NCCR yamfukuza uanachama Kafulila na wenzake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Dec 17, 2011.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chama cha NCCR mageuzi kimemfukuza uanachama mbunge wake David Kafulila. Kwa uamuzi huo uliofikiwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho muda mfupi uliopita huenda akapoteza kiti cha Ubunge. Salama ya Kafulila kuendelea kuwa mbunge ni kwenda mahakamani au kukata rufaa ngazi ya juu ya chama hicho. Hatua hiyo itategemea uharaka wa chama chake kutoa taarifa rasmi kwa Spika wa Bunge, msajili wa vyama vya siasa na Tume ya Uchaguzi kutangaza kiti hicho kuwa wazi.

  Habari kutoka ndani ya mkutano huo kinaeleza kwamba pande zote mbili kwa sasa kila mmoja unapanga mikakati ya kuwahi mahakamani jumatatu asubuhi. Upande wa chama hicho kinachoongozwa na James Mbatia wanakusudia kufungua kesi ya kumzuia Kafulila kuendelea kukishambulia chama hicho baada ya kufukuzwa uanachama pamoja na kumtaka atumie taratibu za kikatiba za chama hicho ikiwapo anataka kukata rufaa. Upande wa Kafulila unaelezwa kuwa umedhamiria kufungua kesi ya kupinga kufukuzwa uanachama ikihoji uhalali wa mkutano huo na taratibu zilizotumika kumuondoa uanachama.

  Awali mkutano huo ulitawaliwa na vuta nikuvute kuhusu taarifa ya mkutano huo, huku upande wa Kafulila ukiwakilishwa na Hashim Rungwe ukikutana na Msajili wa Vyama vya siasa kupinga mkutano huo kuitishwa kwa dharura na kutaka makabrasha ya mkutano kufika majumbani kwa wajumbe kabla ya mkutano. Hata hivyo, baada ya kupitia katiba ya chama hicho msajili hakuona msingi wa kuzuia mkutano huo wa dharura kufanyika.

  Kabla ya mkutano huo kuendelea mwakilishi mwingine wa Kafulila ambaye ni mbunge mwenzake toka Kigoma wa Jimbo la Muhambwe Felix Mkosamali aliweka pingamizi lingine kuhusu wajumbe ambao walielezwa kuwa pandikizi. Hata hivyo, msajili wa vyama vya siasa alitoa orodha ya wajumbe waliopo katika ofisi yake yake ambao ilikuwa na majina ya wajumbe hao. Vyanzo kutoka makao makuu ya NCCR Mageuzi vinaeleza kwamba baada ya mgogoro kuanza Mbatia alitumia mamlaka yake ya katiba kuteua wajumbe hao na kutoa taarifa kwa msajili wa vyama vya siasa. Hata hivyo upande wa Kafulila haukuwa unafahamu kuhusu wajumbe hao wapya hali ambayo ilileta mzozo katika ukumbi huo.

  Katika eneo la ukumbi walionekana walinzi wa chama hicho wakivinjari, lakini kutokana na mzozo huo Hashim Rungwe alitoa taarifa polisi ambao walifika kwa wingi na kukuta tayari walinzi hao wamewatuliza wajumbe wa mkutano na kikao kinaendelea.

  Habari ndani ya ukumbi wa mkutano huo zinaeleza kwamba mara baada ya ufunguzi wajumbe walijadili taarifa ya hatua zilizochukuliwa kuhusu tuhuma zinazomkabili Mbatia. Kutokana na barua ya kumtaka ajiuzulu iliyosainiwa na kundi la Kafulila ilibidi halmashauri kuu ya NCCR Mageuzi impe nafasi mwenyekiti ajieleze. Kutokana utetezi huo wajumbe walipiga kura ya kutokuwa na imani na mwenyekiti ambao wajumbe 42 walipiga kura ya kuwa na imani wakati wajumbe 9 walipiga kura ya kutokuwa na imani na mwenyekiti.

  Baada ya wajumbe wengi kuonyesha kuwa na imani na mwenyekiti mkutano uliamua kujadili kuhusu waliowasilisha tuhuma hizo dhidi ya mwenyekiti wa kiongozwa na Kafulila. Kila mjumbe aliulizwa msimamo wake baada ya kura hizo na Kafulila alieleza kwamba naye ana imani kubwa na mwenyekiti. Kutokana na kauli hiyo kutofautiana na barua aliyoandika kwa wajumbe pamoja na ushahidi wa magazeti mkutano ulimuhoji kufafanua na alisisitiza kwamba ana imani na mwenyekiti isipokuwa magazeti yamekuwa yakimnukuu vibaya. Aidha Kafulila asisitiza kwamba barua ya kujiuzulu mwenyekiti haikuwa ya madai ya kutokuwa na imani naye bali ni changamoto kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.

  Mkutano uliamua kuwatoa wajumbe wenye tuhuma mbalimbali kwa ajili ya kuwajili ambao wajumbe kwa kauli moja waliona kwamba ipo haja ya kuwapa adhabu ya kuwavua nafasi mbalimbali za uongozi. Hata hivyo, wakati kikao kikiendelea likaja kundi lingine la askari polisi ambao walieleza kwamba wamepigiwa simu na Zitto Kabwe kwa ajili ya kuzuia vurugu zilizokuwa zikiendelea katika mkutano huo. Kutokana na madai hayo, mkutano huo ulilazimika kumuita tena Kafulila na Hashim Rungwe ambao walitajwa kuwapokea askari hao kueleza msingi wa kuhusisha vyombo vya dola na watu wa nje wa chama hicho katika mkutano wa ndani wa chama hicho.

  Baada ya kuitwa kwa mara ya pili mbunge wa Kasulu Aggripina Buyogela aliwaomba radhi wajumbe kuhusu uasi huo kutoka katika mkoa wa Kigoma kwa kuwa Kafulila, Rungwe, Mkosomali na Machali wote wanatoka katika mkoa mmoja na yeye. Aggripina aliwaomba wajumbe kutoa adhabu inayostahili bila kutazama mkoa kwa kuwa si watu wote wa mkoa ni wakosaji ili kudumisha nidhamu katika chama.

  Kufuatia kauli hiyo Kafulila akaongezewa mashtaka mengine ya kutoa tuhuma kwa viongozi wenzake na chama kupitia vyombo vya habari badala ya vikao vya chama. Kafulila alidaiwa kufanya vitendo hivyo hata baada ya kuonywa na katibu mkuu wa chama hicho. Baada ya kusikiliza utetezi wake ndipo wajumbe walipiga kura ya kumfukuza uanachama kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama hicho huku wajumbe 8 wakiacha kupiga kura.

  Kufukuzwa uanachama kwa mbunge huyu kumeendeleza wimbi la wabunge kufukuzwa na vyama vyao toka mfumo wa vyama vingi ulipoanza. Miaka michache iliyopita walifukuzwa wabunge wa viti maalum wa CUF ambao hata hivyo walishinda kesi na kuendelea kuwa wabunge kwa amri ya mahakama kutokana na chama hicho kutokufuata taratibu. Wabunge wengine waliofukuzwa ni wa majimbo wa chama cha UDP ambao kutokana na katiba ya chama hicho kufuatwa walipoteza nafasi za ubunge wao licha ya kwenda mahakamani.

  Kafulila alihamia NCCR Mageuzi baada ya kuvuliwa cheo cha uafisa habari wa CHADEMA. Kufuatia hali hiyo aliamua kujivua uanachama na kujiunga na CHADEMA na kuungwa mkono na Zitto Kabwe na hatimaye kushinda uchaguzi wa Kigoma Kusini. Wakati wa uchaguzi na mara baada ya uchaguzi gazeti la Mwanahalisi limekuwa likitoa mfululizo wa habari zikinukuu mawasiliano ya barua pepe baina ya wanasiasa hao vijana machachari zikieleza mpango wa kuichukua NCCR Mageuzi ili kujenga chama kitakachokuwa makini zaidi ya CHADEMA kwa ajili ya kuiondoa CCM madarakani mwaka 2015. Kutokana na habari hiyo vyombo vingine vya habari vimekuwa vihusisha mgogoro wa NCCR Mageuzi na suala hilo hali iliyopelekea wanasiasa hao kukanusha. Hata hivyo, Mbunge mwingine wa NCCR Mageuzi Machali alijitokeza karibuni na kuthibitisha madai hayo huku akidai kuwa ana ushahidi wa mawasiliano yake na Kafulila yenye kuonyesha kwamba alimshawishi kushiriki katika mpango huo.

  PM


   
 2. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mery Christmas Kafulila!!
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Namshauri ahamie kwa Mtikila au John Cheyo aimarishe vyama hivi.
   
 4. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli basi Kafulila alistahili hiyo adhabu.
   
 5. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Kafulila amefulia
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Rudi CDM uombe msamaha kama mtoto mpotevu.
   
 7. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Cha moto amekipata, sijui ataenda wapi?
   
 8. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duu! Kama siamini vile au usingizi nini? Tutaonana alfajiri.
   
 9. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Kafulila na wenzake, kina nani hao sasa Wenzake?
   
 10. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,254
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Mbatia hafai hata kidogo!
   
 11. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kafulila kelele nyingi kwenye kikao kanywea kama mkate kwenye chai, kweli cheo kitamu ananikumbusha mzee Sitta alivyonywea NEC. Ana laana ya CDM, mwache aanze kuhangaika kwa Mapilato.
   
 12. lukenza

  lukenza Senior Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bora imepita salama
   
 13. O

  One tsh. Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Massikini kafulila amepishana na posho!!
   
 14. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Anakazi moja tu kujirekebisha, kwa namna ya pekee.
  Kwani kila anapoenda kuzusha rabsha itakula kwake
   
 15. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kafulila unazikosa lak2,,,hiv hiv
   
 16. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  kigoma kuna nini? Nashauri arudi CHADEMA na kuomba msamaha
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hivi Zitto anahusika nini na mkutano wa NCCR? sometimes huwa simwelewi.
   
 18. melxkb

  melxkb JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AMPIGIA MAGOTI MBATIA KWA MACHOZI, WAJUMBE WAKATAA KUMSAMEHE

  CHAMA cha NCCR- Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urasi wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.

  Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu Nec ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi...


  SOURCE: Mwananchi News Paper


  Big mistake made by NCCR or...................?, No mediation process, just like "KUVUA GAMBA", anyway, don't know how does the NCCR constitution address this?
   
 19. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh Sisimizi Kafulia
   
 20. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Ataanza kuamini maneno ya CHADEMA. kweli jamaa ndo ukweli umedhihilika kwamba yeye ni kama nzi. ataenda mahakamani na kesi etaenda hadi 2014. so anaweza poteza mwaka mmoja. ova
   
Loading...