Chama cha NCCR-Mageuzi kimezindua ilani yake ya uchaguzi kwa mwaka 2025–2030 iliyobeba vipaumbele 11, ikiwemo upatikanaji wa katiba mpya.
Pia, chama hicho kimetangaza wagombea wake kwa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano, Haji Khamis, na mgombea mwenza, Dkt. Eveline Munis, pamoja na mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Laila Rajabu Khamis.