NBA AllStar 2019, Charlotte; King James Ampokonya Curry U-Captain wa East

alvinroley

Member
Sep 30, 2016
71
251
James (Lakers) amekuwa captain ktk allstars kadhaa akiwa Eastern Conference ambazo amecheza dhidi ya Western Conference. Sasa ameteuliwa kuwa nahodha wa kanda ya Magharibi kwenye NBA All-star 2019 huko Charlotte baada ya kuhamia Lakers iliyopo kanda hiyo ambayo kwa Mara kadhaa imekuwa chini ya unahodha wa Stephen Curry (Warriors). Kwa maana hiyo Curry atashiriki All-star ya mwaka huu chini ya uongozi wa LeBron huku kanda ya Mashariki wao wakiongozwa na Giannis Antetoukunpo kutoka Milwaukee Bucks ya jimbo la Wisconsin. Je James ameonekana ni bora dhidi ya Curry? Au ndio ukweli wa ile Debate iliyokuwa ikiendelea mwishoni mwa mwaka jana huko Marekani kuwa Durant ameuzorotesha u-leader au ufalme wa Curry pale Oakland?
_20190131_181820.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
le bron ndio face ya nba kwa decade hii... imefika kipindi wachambuzi wanamlinganisha na jordan..

curry ni mtoto mdogo sana kwa level ya lebron james..

le bron hata university hakwenda.. ila akawa namba one pick nba draft straight from high school.. na hapo vyuo vyote vikubwa vilimpa scholarships akagoma...

curry wakati anatoka high schools hata top university zilimkatalia kiwango chake kidogo

akaenda chuo kidogo davidson,,, na huko curry akakaa college miaka mitatu anacheza kikapu.. hata robo fainali ya college hakuwai kufika..

curry bila kuungana na durant.. hata rings alizopata miaka hii asingezipata..

lebron timu yeyote atakayocheza lazima isumbue hata kama wengine makapi... hata lakers hii ya madogo.. kwenye playoffs haitakosekana na itasumbua sana .. lebron akiwa health
 
Back
Top Bottom