Nazi zimepanda bei au ni double standards kwenye HUKUMU?

shizukan

JF-Expert Member
Jan 16, 2011
1,158
563
Kwenye magazeti ya Ijumaa iliyopita, mojawapo limeandika habari za kufungwa jela miaka miwili jamaa mmoja huko Zanzibar (somebody Athumani) kwa kosa la kuiba nazi 10 ktk shamba la makamu wa rais Shaababi Gharib Bilal. Nilichokishangaa mimi ni kupewa hukumu sawa na huyu jamaa yetu asiyeweza kutulia Segerea bila SIMU ambaye yeye soo lake ni kubwa la mamilioni.

Kwa kifupi huu ni uharibifu wa fedha za umma kumlisha Athumani msosi wa bure kwa kuiba nazi 10. Badala yake Athumani angetafutiwa adhabu mbadala inayohusika na kazi ili ajifunze kuwajibika badala ya kumpa kifungo equivalent na mheshimiwa aliyetuibia 'beautifully'
 
wizi ni wizi kisheria adhabu ni ile ile kama imeanishwa kwenye minimum sentence act hakimu
hawezi kupunguza kama zanzibar hawana hiyo basi hakimu angetumia busara walau faini kidogo au adhabu ndogo zaidi

Kinachoadhibiwa ni kosa. Quantity may not be important in determining the sentence. It may be a mitigating factor though!
 
Hata mimi sikusema sheria haipo, ninachokishangaa mimi ni hiyo hiyo sheria. Kama hai-reflect mahitaji ya jamii basi haina maana kwetu. Mtu aliyeiba nazi dhahiri anaongozwa na njaa, kwa hiyo kumfunga na kumuachia baada ya miaka miwili hakumsaidii yeye wala jamii yake, ndio maana nikasema angepewa adhabu mbadala ya kumfanya awe muwajibikaji. Vivyo hivyo, aliyeiba mamilioni ilhali ni mtumishi wa umma, hatuwezi kusema ni njaa, tayari ana kazi yenye kumpatia kipato chenye kukidhi mahitaji muhimu ya maisha kwa hiyo ni tamaa tu ndio inamuongoza kuiba, kwa hiyo mtu wa namna hii anastahili adhabu kali. Sasa ukiniambia mwizi ni mwizi tu, hoja yako inakosa mantiki ya kwa nini tuna magereza: kuwabadili watu tabia au kulitia taifa gharama.
 
Kinachoadhibiwa ni kosa. Quantity may not be important in determining the sentence. It may be a mitigating factor though!

Kosa haliadhibiwi, anayeadhibiwa ni mtenda kosa. Hapa sikusema nazi kumi sio kosa, bali nilichokiangalia kwa nini mtu kaiba nazi kumi. Madhara yanayopatikana kwa wizi na namna hii hayalingani na gharama za utoaji wa adhabu kwa kosa la namna hiyo, kwa hiyo yanakosekana manufaa kwa mkosaji na taifa pia. If we think in a more positive way, sheria zetu zilipaswa kutusaidia kujenga jamii bora na sio kutugharimu pasina sababu za msingi. Mwizi anayeiba akiwa ofisini haitaji consultation, ni adhabu itakayomuonesha ubaya wa tamaa, lkn mwizi wa nazi, anahitaji special consideration aweze kubadilika, kiuchumi na kimtazamo.
 
wizi ni wizi kisheria adhabu ni ile ile kama imeanishwa kwenye minimum sentence act hakimu
hawezi kupunguza kama zanzibar hawana hiyo basi hakimu angetumia busara walau faini kidogo au adhabu ndogo zaidi

Wanao iba kwa makaratasi mbona wanafungwa kifungo kidogo?
 
Back
Top Bottom