Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,429
Habari wanajamvi,
Maoni yenu na ushauri wenu ni wa muhimu sana kwangu kwenye hili;
Mimi nimeajiriwa nafanya kazi na kulipwa mshahara wa hali ya kawaida. Sio mdogo na wala sio mwingi bali unatosha kusongesha maisha. Mume wangu yeye amejiajiri kwenye sekta ya video shooting na upigaji picha kwenye sherehe mbalimbali na pia anafanya kazi za graphics design.
Sasa kuna wakati au msimu kazi anazopata huwa zinakuwa chache sana au wakati mwingine anakuwa hapati kabisa kazi kwa muda fulani. Na inapofikia hali hii uchumi wake unayumba sana ukizingatia kwamba yeye ni baba wa familia na huwa anajisikia vibaya sana anapokuwa anapitia kipindi hiki jambo ambalo huwa linaniumiza kwa sababu anaona kama vile mzigo mkubwa wa majukumu ya familia unakuwa wa kwangu mimi mama.
Je nawezaje kumsaidia ili hali yake ya kipato isiwe inayumba hata pale anapokuwa hapati kazi za kufanya kwenye hiyo sekta ya kupiga picha na video?
Natanguliza shukrani kwenu wote mtakaonishauri vizuri.
=====
Mada hii imetumika ktk JamiiLeo