maonomakuu
JF-Expert Member
- Jul 24, 2015
- 2,516
- 1,198
Wakuu kila mtu na zama zake bana
Mwinyi alipomaliza muda wake alisemwa vibaya sana kwamba kaharibu uchumi na kuleta ubepari.
Mkapa alipomaliza alitukanwa sana kwa ufisadi mbalimbali mfano kufanya biashara na mkewe ikulu na ubinafsishaji wa mashirika ya umma. Alisemwa vibaya kana kwamba hakuna alichofanya.
Maskini Rais wangu Kikwete leo kila mtu anamwona hana maana yeyote wala alama ya kukumbukwa wakati kafanya mengi mema na alikuwa na huruma kwa wananchi.Tusisahau kadiri miaka inavyokwenda administration ya binadamu inakuwa ngumu zaidi hata Nyerere angekimbia utawala wa leo.
Leo tuko na Magufuli anasifiwa kila kona na ukimsema vibaya au udhaifu wake basi utaonekana wa ajabu. Amekaa vizuri kwenye mioyo ya watu kama Kikwete kipindi cha awamu ya kwanza.
Tuwe wapole jamani Wana CCM acheni kumwona Kikwete hafai kabisa japo mlimlamba miguu alipokuwa Rais.
Magufuli asipokuwa makini anguko lake litakuwa kubwa kuliko Kikwete. Tuwashauri na pia tuwakosoe wanapokosea
NAWAZA TU