Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Nimemsikia Raisi mstaafu Kikwete akisema kwamba Wazungu wanajukumu la kutusaidia kwa kuwa eti walitunyonya na kwamba uchumi wao umejengwa kwa mali za Afrika hayo ni maneno ya Kikwete siyo yangu, Kikwete amerudia maneno ambayo Mlm.Nyerere ndiyo alikuwa anapenda sana kuyatumia na Nyerere aliamini kabisa kwamba Wazungu wanajukumu la kutusaidia nafikiri na yeye (Nyerere) alipotoshwa na watu kama Walter Rodney aliyeandika kitabu cha ,,How Europe Underdeveloped Africa", na fikra kama hizi ndizo zilizoongoza Siasa za Mlm.Nyerere na ambazo tumekuwa tukizirithi tawala hadi tawala mpaka kwa Kikwete fikra zilizosababisha nchi yetu kuwa nchi inayotegemea misaada klk nchi zote Afrika, hakuna nchi inayopokea misaada hapa Afrika kama yetu!
Sasa kwa nini nawapinga (Nyerere, Kikwete & Co.)? Ni kwamba siyo kweli Wazungu au Ulaya imeendelea kwa sababu ya kunyonya Afrika!
Ulaya walikuwa na Makoloni Dunia nzima kwanza kwa nchi kama Uingereza Afrika wala haikuwa Koloni lake muhimu, grand colony la Uingereza lilikuwa ni India, huko ndiko kama ni kusema Wazungu waliiba basi ni India, Waingereza walikaa India miaka 150 na Mapinduzi ya viwanda yalioanzia Uingereza yalichangiwa na India kumbuka Mapinduzi ya viwanda yalianzia na viwanda vya nguo ambavyo mali ghafi ilikuwa inatoka India, Waingereza wamekuja Afrika kwetu mwishoni kabisa na ilikuwa ni extension ya India tu!
Uingereza kama zilivyo nchi nyingine za ulaya imetawala Marekani ya leo na huko kote walikuwa wanachukuwa malighafi na kupeleka kwao kujenga Viwanda vyao mpaka Marekani walivyogoma na kuingia vitani, vita iliyoleta Uhuru na kuzaa USA!
Hivyo kusema kwamba Wazungu ni lazima watusadie kwa kuwa walitajirika na malighafi ya Afrika siyo kweli na upotoshaji!
Tuchukulie mfano wa nchi yetu ambayo ilitawaliwa na Wajerumani, sasa Wajerumani walichukuwa nini TanZania? Kwanza unaweza kusema waliwekeza klk walivyochukuwa kama ukipiga mahesabu ya Miundo mbinu waliyojenga kama Reli, Br, Mipango miji Miji yote ya TZ ambayo tunaishi ilipangwa na Wajerumani hata kilimo, kuamua wapi tulime Kahawa, Chai, Mkonge au Mahindi na Pamba utafiti ulifanywa na Wajerumani kwa kutumia Chuo cha Utafiti walichokijenga kilichoko Lushoto Tanga ambacho leo tunakiita Amani institute hiki kilikuwa Chuo kikubwa cha utafiti Duniani kilipokamilka na ndicho kilichotoa majibu ya kuleta Katani Tanzania ktk Mexiko, kulima Pamba Mwanza, Kahawa kagera, Moshi n.k
Hata haya madini tunayochimba leo kama dhahabu au pia Gesi asilia kila kitu kilifanywa zamani na Wazungu ramani zipo tunachofanya ni kurudia tu lkn kila kitu kipo, sasa hawa Wazungu walichukukuwa nini? Hata Ziwa Tanganyika meli pekee inayohudumia Ziwa hilo tuiitayo MV. Liemba iliwekwa na Wajerumani karibia miaka 100 iliyopita ni nani aliwalipa hiyo gharama?
Rejea Wajerumani walikaa hapa kuanzia kama 1890 - 1918 na muda wote huwo walikuwa wanawekeza tu baada ya hapo wakaja Waingereza ambao tayari walikuwa wameshaendelea na wameshachoshwa na Makoloni na waliiba nini ktk kwetu? Kwa maana kama ni Almasi ya Mwadui Nyerere ndiyo aliyewapa Williamson baada ya Uhuru, Kama ni dhahabu na Gesi yetu ni Mkapa na Kikwete ndiyo walioigawa kwa wageni!
Hata samaki ya Sangara ambao ndiyo moja ya export yetu kubwa ktk Ziwa Viktoria walipandikizwa humo na Wazungu hao Samaki siyo asili ya hilo Ziwa, lkn ndiyo wanaochangia kiasi kikubwa cha exports zetu leo hii!
Hata hii DART tunajenga leo Ramani ipo tangu Ukoloni, hakuna jipya hata limoja!
Hivyo basi kusema kwamba sisi tunastahili kusaidiwa kwa sababu Wazungu wameendelea kwa sababu yetu ni kutafuta visingizio, kwa nini sisi tu?
Indonesia ilitawaliwa na Uholanzi ilijulikana kama Dutch East Indies mbona Waindonesia wako mbele kimaendeleo na hawalii kwamba ni lazima wasaidiwe na Wazungu? Rejea kwamba Indonesia imetawaliwa na Wazungu kuanzia mwaka 1600 mpaka mwaka 1945 kwanza na Waholanzi halafu Wajapani sasa kulinganisha na sisi Wazungu wamekaa muda gani kwetu? Wajerumani kuanzia kama 1890 -1918 Waingereza kuanzia hapo mpaka 1961 hata miaka 100 haifiki iweje sisi tulie kuomba msaada wakati Indonesia waliotawaliwa miaka zaidi ya 300 hawalii na wamejipanga leo wanaendelea?
Siyo sisi peke yetu tuliyotawaliwa Brazili ilitawaliwa na Ureno kwa miaka mingi sana, Korea walitawaliwa na Wajapani na Wajapani waliiba Rasilimali nyingi za Wakorea lkn Wakorea hawalilii misaada badala yake wamejipanga na wametoka? Taiwani ilitawaliwa na Wajapani na kote huko Wajapani walikomba Rasilimali kwa ajili ya viwanda vyao mbona Taiwani hawalii na kuomba misaada ktk Ujapani? Mbona wao wameendelea?
Hivyo namalizia kama nilivyoanza kwamba napingana na Nyerere, Kikwete &Co. wanaposema kwamba Wazungu wanapaswa kutusadia kwa sababu wameendelezwa na Afrika hilo siyo kweli hasa ukichukulia Historia ya Tanzania kwani kama kweli ni swala la kuiba Rasilimali hapa kwetu waliiba Waarabu hao ndiyo waliokaa hapa muda mrefu klk yoyote yule na siku zote walichukuwa Rasilimali kuanzia Watumwa mpaka mali nyingine mbona hatuwaombi hao misaada kwa nini tunasema Wazungu ndiyo walioiba ili hali Wazungu hawajakaa hata miaka 100 hapa kwetu?
Hivyo namuunga mkono Raisi Magufuli kwa kuanzisha Tanzania mpya na kuizika ile ya Mlm.Nyerere ambayo nina imani imekomea kwa raisi Kikwete hasa kwenye upande wa misaada kwamba hatuhitaji misaada sisi siyo binadamu nusu bali ni binadamu kamili kama wengine na tunaweza kuendelea kama wengine walivyoendela kwa kutumia rasilimali watu na kuendelea!
Viva Raisi Magufuli wewe ni TanZania mpya, wewe ni Afrika mpya!
Picha ya Chuo cha utafiti Amani wakati wa Uhai wake 1903-1908 hapa ndipo majibu ya kilimo cha Katani yalipotoka, na leo hii sisi ndiyo nchi yenye katani nyingi Duniani, siyo Katani tu Pamba, Kahawa, n.k!