MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Furahieni kwa wapinzani kufungwa kwa kesi kubambikia, kesi za kisiasa, kesi zisizoeleweka.Hawa wote wana wana damu,wana familia na ndugu wengine wanao wategemea katika maisha yao, ninyi chekeleeni lakini yana mwisho haya.
Watu wanafungwa kwa sababu tu wamefanya mikutano ya kisiasa ilihali ipo kisheria, watu wanafungwa kwa sababu ya kujibizana na polisi kwenye vikao! Mtu yuko mahabusu kwa sababu tu ameota kitu flani ambacho hakuna mwenye uhalisia nacho.
Niseme tu wazi kwamba malipo ni hapa hapa duniani, Mungu hulipa hapa hapa kabla ya kurejea kwake. Iko siku yatawageukia haya maana hakuna aijuaye kesho yake. Hakuna Chama kinachoweza kutawala milele duniani.