Tanzania Land Authority inahitajika ku-control bei za ardhi.
bei ya kawaida sana kwa ununio....kikwete mwenyewe amejengewa nyumba ya kustaafia uko...wewe unataka kuwa jirani na Jakaya kwa kununua kiwanja kwa laki sita sio....
Mmh ila ununio ni bado uswahilini sana ni kiwa na maana ukileta ujuaji wazee lazima wakutulize kwa mambo yetu yale ya techonology kuna jamaa yangu kajenga huko sasa hivi anataka kuuza
ununio ipi?
kama ni pale stand kuelekea beach kule kweli ni uswazi (unsurveyed) wanakaa wazawa very local
viwanja vipo upande wa pili wa barabara ya lami kama unaelekea basihaya huku ni surveyed plots only na hakuna mambo ya ajabu kama kule uswazi maana mitaa ya huku kila mtu kajifungia getini.
Tanzania Land Authority inahitajika ku-control bei za ardhi.
Ni kama vile mtu anakurupuka tu, hakuna cha kusema kwa square meter moja kinauzwa kiasi gani wala nini..unajuwa humu kuna watu aise wanasaidia sana na wanazo info kuhusu viwanja..
Dar Property Home
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-biashara-na-uchumi/514948-bei-za-nyumba-maeneo-ya-dar.html
Sasa Tegeta Ununio ukiuza viwanja kwe bei hio, Kijitonyama utauza kwa shs. ngapi?!
Hivi hiyo mamlaka ipo kweli?
Nakubaliana na wewe kwamba hii bei inaweza kuwa kubwa sana kwako lakini kama kweli hicho kiwanja kiko maeneo ya Ununio hasa ile mitaa ya karibu na Beach au barabara ya lami, kumekaa vizuri sana na viwanja ni vikubwa, hakuna uswahili, kumepimwa na kila mtu kajifungia getini kwake. Huduma karibu zote zinapatikana kwa urahisi hasa maji ambayo suala la kukatika hovyo sio kawaida sana. Tena kwa mjasiliamali wa uhakika anaweza tengeneza kitegauchumi cha nguvu na akarudisha hela yake ndani ya muda mfupi sana.
Jambo la msingi, kabla hujafikiria kununua au kubeza hiyo bei fika uione location then argue based on your research evidence. Ni ushauri tu kama mkazi wa maeneo hayo!