Nauza nyumba Kigoma


Nop!! Mimi nafanya kazi kigoma kwenye ishu za wakimbizi kwa sasa nakaa Nolad.
 
Wewe kweli ni mwenyeji,, barabara ipo na inapitika siku 365/6, nilikuwa na kigari mfano wa vits na kalikuwa kanapanda tu bila shida.

Kiwanja ninacho pia, maeneo ya juu ya Kigoma secondary, ni Low density pia kiko mlimani. ukinipa 10 mil nakuachia.
basi kwa hapo mambo mazuri nyumba nzuri.
Unajua mji mwema ni sawa na Oysterbay kwa hadhi ya Dar.
Vipi hicho kiwanja cha mji Juu ya Kigoma Seco kinaangalia Ziwa au?Maana nilikuwa napenda Maeneo ambayo unapata view ya Ziwa kama hapo kwako.
Mungu akipenda nataka baada ya miaka miwili nijenge huko,unajua mie mwenyeji na mzaliwa wa huko.Nilisomea pale Kigoma Primary jirani na shule ya kiezya kisha nikaingia Kigoma Secondary mwaka 1994 ambapo Zito Kabwe alikuwa Kaka mkuu.Then nikaanza kukatambuga kama swala pala kutafuta maisha.

Kigoma mji mzuri sana ila pesa ngum kupita maelezo,Kuna ndugu yangu alikuwa na nyumba tatu mji mwema zote UN wamezikodi yeye yupo Dar anakula bata,yaani pesa nzuri sana.
 
Kiwanja chako kina hati na kimehakikiwa na watu wa Ardhi?? Kuna jamaa yangu aliwahi kuuziwa kiwanja fake na wale madalali njaa wa Ujiji
 
Kiwanja chako kina hati na kimehakikiwa na watu wa Ardhi?? Kuna jamaa yangu aliwahi kuuziwa kiwanja fake na wale madalali njaa wa Ujiji

Kina haki mkuu, mimi sio dalali na kiukweli sipendi kuwahusisha madalali
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…