Nauza mti wa Mvule

Hapana ni wake kabisa, ila ili kuwa salama na kupata haki yake stahiki atafute Kibali cha kuuvuna. Anzia na ofisi ya kijiji / mtaa, maana hao ndio wanaujua mti na wewe wanakujua. Watakuandikia barua kupeleka ofisi ya maliasili halmashauri. Hao maliasili watakuelekeza zaidi ikiwa pamoja na malipo unayopaswa kulipa.
 
Nimekupata mkuu wangu. Wacha nichacharike kuupiga bei fasta
Utapata hasara, Mvule ni mti wa mbao ngumu na nzuri sana. Bei yake ni nzuri sana pia. Uchane wewe mwenyewe.
Angalizo: kama uko kwenye chanzo cha maji, au kwenye mteremko hautaruhusiwa kuuvuna. Kwa sababu utakuwa unahifadhi chanzo au utakuwa unazuia mmomonyoko wa udongo.
 
Hapana mti haupo kwenye chanzo cha maji wala mtemko ni eneo tambarare.

Sasa kuchana mbao si gharama tena mkuu? Na uuzaji wa mbao zenyewe kuanza kuzunguka mjini kutafuta wanunuzi?
Gharama ya kuchana haitakuwa kubwa kuzidi mauzo. Wateja ni hao wenye karakana za seremala. Patana nao kabisa. Ukiwa na vibali haraka sana watachukua. Mbao za Mvule ni nzuri sana, "hazigongwi" na wadudu. Jaribu kuulizia mlango wa Mvule usikie bei yake.
 
Fuata kwa tahadhari ushauri wa hawa watu. Ukibisha endelea. Wewe sio mfanyabiashara wa mbao na itakuwa too cost kukata vibali kwa mti mmoja tu. Hao wafanyabiashara wakikuta umeshachana watatoa kasoro mia kidogo;kwani watakuwa wanajua huna ujanja huku ushaingia gharama kibao. Watakwambia mvule maji, mvule mvua mvule matope nk nk.
 
Hapana mti haupo kwenye chanzo cha maji wala mtemko ni eneo tambarare.

Sasa kuchana mbao si gharama tena mkuu? Na uuzaji wa mbao zenyewe kuanza kuzunguka mjini kutafuta wanunuzi?
Mkuu huo mti ukiwa hapo shambani utaathiri shughuli zako zozote au unakukera ukiwa hapo? Kama hauathiri basi uache ukae hapo sababu hiyo thamani uliyonayo kama unatunza mazingira. Tujaribu kutunza mazingira na vyanzo vyake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…