Nauza mabati, nimenunua yamezidi

ugali dagaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
1,284
Reaction score
1,128
nimeshayauza asante jf mod nisaidie kufuta hii thread
 
mleta mada mimi sihitaji mabati ila nakupa hongera kwa huo mjengo hongera sana mleta mada
 
mleta mada mimi sihitaji mabati ila nakupa hongera kwa huo mjengo hongera sana mleta mada

Hahahaha,aisee angalua nimecheka leo.
Unajua nyumba ukiishaanza kuezeka ndio show yake inaanza kujijenga,hasa ukipata wenye kujua kunyoosha na aina ya bati kama hizo.
Na kwa joto la Dar nyumba lazima iwe ndefu kama hivyo
 
Pole...
Naddhani iwe funzo kwa wengine mnaokwepa utitiri wa wataalamu mtaani kwa kukimbilia urahisi...Yumkini hata ramani ulipewa tu na fundi! Siku nyingine,hata kama sio wewe mshauri rafiki yako ama mwanao amwone msanifu majengo,mkadiriaji wa gharama za majenzi,mhandisi, na wataalamu wengine ili kuepusha mikanganyiko inayozuilika...
 
mita sita na nusu ziko mbili, mita nne na nusu ziko tano mita tatu liko moja mita mbili yako mawili mita moja na nusu yako kumi

Aisee huyo fundi aliye overestimate ulimchukulia hatua gani? Manake hiyo sasa ni too much...

Au alitaka akuibie ukamkaba vilivyo. Mafundi wengine nuksi sana
 
Aisee huyo fundi aliye overestimate ulimchukulia hatua gani? Manake hiyo sasa ni too much...

Au alitaka akuibie ukamkaba vilivyo. Mafundi wengine nuksi sana

ni fundi mzoefu kama ulivyosema alikuwa na lengo la kimaksudi ila nilihakikisha nasmamia kazi mpaka mwisho hivyo akashindwa kutimiza azma yake hiyo ovu....tumekubaliana tuyauze mabati ndio nimmalizie labour charge......
 
Pole mkuu ungekuwa sio mfuatiliaji ungeambiwa yamepungua 10!
 
Unataka tuwaone hao wataalamu wako sijui wa kukadiria majenzi,sijui waandae B.O.Q ili gharama za ujenzi ziwe juu si ndio?
Watu tunajitahidi Ku minimize cost to the lowest as possible afu wewe unashauri nini sijui.

Na hivi sheria ya manunuzi inaangaliwa upya,wengi mtaisoma namba.
 
ni fundi mzoefu kama ulivyosema alikuwa na lengo la kimaksudi ila nilihakikisha nasmamia kazi mpaka mwisho hivyo akashindwa kutimiza azma yake hiyo ovu....tumekubaliana tuyauze mabati ndio nimmalizie labour charge......

Duh.... bora umekaba vinginevyo angekuja na hesabu ya "kukadiria vibaya" ukaambiwa yamepungua. Mafundi bana....
 
Hongera kwa mjengo, mafundi wa Bongo muda wote akili yao wanawaza kukuliza tu, hiyo ni hasara kubwa, lakini hope utayauza.
 
mita sita na nusu ziko mbili, mita nne na nusu ziko tano mita tatu liko moja mita mbili yako mawili mita moja na nusu yako kumi
Ingekuwa pieces zote zinafanana size ingekuwa rahisi kununulika. Anyways.. huenda akatokea mtu atakayehitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…