Habari ya jioni waungwana. NINATAFUTA kampuni inayonunua vigae ..yaani chupa zilizopasuka,vioo vya milango n.k, nina tani kama 20 hivi, nilifanya biashara hii yakukusanya hivyo vigae bila kuwa na taharifa za kutosha wapi pa kuuza, japokuwa nilifahamu wanunuzi mojawapo ni KIOO LTD, sasa nimeenda ofisini kwao nikaambiwa niandike barua alafu nitajibiwa.
Imepita miezi 2 sijajibiwa. sasa naomba kuuliza kama kuna mtu mwe ufahaam zaidi soko la vigae lilipo na bei yake anijuze.
Niko mkoani Shinyanga.
Nitashukuru sana.