Mda wowote kuanzia sasa nauli za daladala zitapanda ili kukidhi hari halisi ya uendeshaji na gharama za maisha kupanda. Watanganyika tujipange kwa haya maisha bora ya kwa kila Mtanganyika. Tumedhubutu........., tumeweza............
Ni Bora Mambo kwa Dar Yazidi Kuwa Magumu ili watu wafunguke na Kuanza Kudai Haki!! Kama uboreshaji wa usafiri wa Jumla, Hali bora za Makazi, Huduma bora za Maji safi, Miundombinu ya barabara nk,nk,.....
natamani nauli ipande maradufu,umeme ukae ivo ivo kimgao mgao na bili inakuja hata kama umeme na maji yamekatika,apo ndo wanambagala,temeke na ilala watakapopata akili ya kumchagua mwakilishi mwenye uchungu na wananchi...wamethubutu,wameweza na wazidi kusonga mbele!
Inatakiwa ifike kabisa 1,000/=kwa kila ruti moja sababu hawa binaadamu(Watanzania)kwa maneno hawadikii wala kuona Ila vitendo vitawaamsha huko walipolala
na kweli zipande maradufu wadanganyika wamelala sana naona wataanza kutembea kwa miguu hawashindwi ili wasilalamike. aliyeiroga TZ kishakufa so TZ wanaona ni haki yao mateso yote,wk kwn usingizi mzito sn. Chai,Chapati,Mchuzi kidumuuuuuuuuuuuu. Kidumuuuuuuuuuuuu.
Mbona nauli mimi ilishapanda siku nyingi,kuna basi moja lina charge tshs 2000 toka mbezi mpaka posta hivi hiyo haitoshi tu.Halafu hilo basi limewashawishi abiria wanaolitumia basi hilo wajiunge kwenye saccos ya kizushi tu.
Ni lazima tulipie gharama za mkuu wa nchi kutalii Ulaya na kwingineko Barani Africa...Maisha bora kwa kila mtanzania si ndiyo hayoooo wa JF acheni kuchonga ili hali mlichagua ugumu wa maishaaaa