Naibili
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,878
- 1,060
serikali kupitia sumatra wametangaza nauli mpya mwezi huu na zimeanza kutumika tangu tarehe 12/4 l, kwa mujibu wa sumatra ni kuwa kupanda kwa bei kumefuata taratibu zote, hii si hoja yangu.
ushauri wangu:
Nadhani imefika wakati watu wa sumatra waanze kufanya kazi zao kwa ufanisi ili waitendee haki hela wanazilipwa kutokana na kodi zetu,
kuna namna nyingi zinaweza kufanywa na serikali na kupunguza gharama kubwa inayotumiwa na wananchi hasa wa kipato cha chini ambao asilimia kubwa wanaishi chini ya dola moja,
kwanza wanatakiwa kuifungua stend ya makumbusha. hii itasaidia wale wote wanaotumia bara bara ya mandela rd na morogoro rd badala ya kulipa 800 au zaidi watapanda gari moja hivyo kutumia 400, huu ni kama mfano maana zipo stend nyingi zikitumika zinaweza kupunguza nauli zinazo lipwa mara mbili wakati inaweza kutumika nauli moja.
jambo la pili ni kuanzisha ruti mpya, kwa mfano posta-kawe via kibaki rd, kawe-temeke via mandela rd. na nyingine nyingi itawasaidia watu kulipa nauli moja.
jambo la tatu, kudhibiti ukatishwaji wa ruti hasa nyakati za asubuhi na jioni, gari nyingi hubadili ruti na kwenda kwingine huku wakibadili nauli na kufanya kati ya 1000 na 2000 hii inawaumiza wananchi wengi hasa wale wa mbagala, mbezi ya kimara, tangi bovu na tegeta ... n.k,
yako mambo mengi serikali inaweza kufanya bila kupunguza nauli iliyowekwa na wananchi wakapata unafuu, mengine mtaongezea wadau mimi ntaendelea baadae.
naomba kuwasilisha