Usikatishwe tamaa na coment za baadhi ya watu humu, tembea katika malengo yako. Kitu cha msingi ni kuanza kuwa jirani na wapiga kura wa eneo ambalo umechagua la kwenda kuwawakilisha wananchi wako., kikubwa kabisa kwenye siasa ni kuwa na goodwill na sio pesa nimesema hivyo kwa sababu umesema kipato chako ni cha chini mno. Tumeshuhudia matajiri wengi wenye pesa waliojaribu kuingia kwenye siasa walishindwa hii ni kutokana na kukosa goodwill.ukiwa na money + goodwill kazi yako inakuwa ndogo sana, ila ukiwa na fedha huna goodwil kufanikiwa kwenye siasa utachukua miaka mingi sana.ukiwa na goodwill huna fedha unaweza kushinda na kuwa mwakilishi mzuri
Hutakiwa kuwa na fedha nyingi sana za kuwapa wapiga kura, ila unahitaji kuwa na fedha za kuwawezesha wanakamati wako(kamati ya ushindi) kwa mafuta, stationary na posho, huku mara zote ukiwa watia moyo kwamba ukifanikiwa mmefanikiwa wote kama itakavyokuwa kwa wawindaji kwamba kila aliyeenda porini kuwinda hata kama mnyama aliyepatikana ni mdogo kila mtu aliyeshiriki hupata kidogo kidogo, ndivyo itakavyokuwa kwenu na kambi yako.kila mwanakamati inatakiwa kuwe na mtu anayemfuatilia ili kubaini ni yupi mpiganaji wa kweli na yupi mamluki, ,kwa sababu kuna baadhi ya wagombea hupandikiza masnitch kwenye kambi za wengine ili kupata taarifa za upande wa pili.mwanzoni unaweza kuwa na kambi kubwa mwishoni unabaki na kambi ndogo.epuka kuunda kambi mapema hii itasaidia kutofirisika mapema.
Ushauri wangu kwako tafuta fedha za kuwezesha kambi yako ya ushindi na si fedha za kuhonga wapiga kura, mpiga kura hahitaji fedha mpiga kura anahitaji goodwil .nakutakia ufanisi mwema katika kutekeleza ndoto yako