Natarajia kuja kugombea ubunge jimboni kwangu

danya

danya

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Messages
3,164
Points
2,000
danya

danya

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2014
3,164 2,000
Habarini.....

Kila mmoja huwa na Ndoto katika maisha yake na hizo humfanya asilale akiwaza namna ya Kufanikisha

Nina Ndoto za Kuja Kugombea Ubunge Jimboni kwangu ndani ya Miaka 5 ijayoo! Nina amini katika elimu ili uweze kuongoza kundi kubwa la watu na uweze kuwa na FACTS katika Kuchangia maada hata kutafuta njia mbali mbali za kuwanufaisha wananchi wako! Japo sifa ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika( Naamini hii iliwekwa kwa wenye pesaa na sheria hii imekaa kirushwa rushwa) Hivyo mimi siku kukubaliana nayo sana! Nikaamua kwenda kusoma Nipate elimu walau niwe na Degree! Sasa nimemaliza kusoma nataka kutimiza ndoto yangu

Mimi si Mwanachama wa Chama chochote hadi sasa na Sijawahi Miliki kadi ya uanachama wa chama chochote kilee hadi sasa! Sijawahi hudhuria vikao vyovyote vile vya kisiasa wala mikutano yoyote ile ya kisiasa! Sijafanya kitu chochote cha kuleta maendeleo jimboni kwangu hadi sasa maana sitambuliki kwa chochote kile zaidi ya kuwa ni mwananchi wa jimbo husika! Sijawahi Hudhuria mikutano ya kijiji wala sijawahi kuongea chochote na viongozi wangu wa kijiji kuhusu maendeleo ya kijiji chetu! Nilikuwa nawaza nipate shule kwanza mengine yatafuata

Sijawahi Piga Kura wala kufanya kampeni ya chama chochote kileee! Sijawahi onesha msimamo aangu kisiasa na Chama nacho kiamini kwasababu nilikuwa natamani nifanikiwe kwanza katika Shule! wazazi wangu hawajawahi kuwa wanasiasa wala wafuasi wa chama chochote kile

Sijawahii jichanganya sana na wananchi wa jimboni kwangu kwa chochote zaidi ya kushiri misiba na harusi pale napoweza sababu ya Shule!

Sasa Nahitaji kugombea Ubunge kwa Miaka 5 ijayoo japo kwa sasa Kipato changu ni chini ya Millioni Moja Kwa Mwezi!

Nipo hapa Kuomba Ushauri,Njia mahususi za kupitia,vitu vya kufanya ili niweze kuja kuwania ubunge na Kushinda! Hii ni ndoto lakini nataka iwe kwelii

Najua hapa Kuna wabunge,Waziri,viongozi mbalimbali na wananchi wa kawaida ambao watanishauri vyema ili ndoto yangu itimie!

Swali Kubwa je nifanyaje ili ndoto yangu ya kuwania Ubunge baada ya miaka 5 itimie?

Nasoma Comments zenu hapa nakujibu maswali pale inapohitajika

Nawasilisha
 
Remote

Remote

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Messages
17,392
Points
2,000
Remote

Remote

JF-Expert Member
Joined May 20, 2011
17,392 2,000
Kama hata hujui njia gani utumie cha kwanza nasikitika!!! Ila labda nikushauri jambo jepesi tafuta kitabu cha Yericko Nyerere "the strategy road to power "
 
e2n

e2n

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2015
Messages
611
Points
1,000
e2n

e2n

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2015
611 1,000
Kwanza kwa maelezo yako tu we we siasa huiwezi na wala haiko kwenye damu. Kama hata baba yako haijui siasa we we utapoteza hela zako bure. Siasa ni darasa refu lisilozoeleka so bora Fanya mambo mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkamanga original

mkamanga original

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2015
Messages
205
Points
250
Age
40
mkamanga original

mkamanga original

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2015
205 250
Usikatishwe tamaa na coment za baadhi ya watu humu, tembea katika malengo yako. Kitu cha msingi ni kuanza kuwa jirani na wapiga kura wa eneo ambalo umechagua la kwenda kuwawakilisha wananchi wako., kikubwa kabisa kwenye siasa ni kuwa na goodwill na sio pesa nimesema hivyo kwa sababu umesema kipato chako ni cha chini mno. Tumeshuhudia matajiri wengi wenye pesa waliojaribu kuingia kwenye siasa walishindwa hii ni kutokana na kukosa goodwill.ukiwa na money + goodwill kazi yako inakuwa ndogo sana, ila ukiwa na fedha huna goodwil kufanikiwa kwenye siasa utachukua miaka mingi sana.ukiwa na goodwill huna fedha unaweza kushinda na kuwa mwakilishi mzuri

Hutakiwa kuwa na fedha nyingi sana za kuwapa wapiga kura, ila unahitaji kuwa na fedha za kuwawezesha wanakamati wako(kamati ya ushindi) kwa mafuta, stationary na posho, huku mara zote ukiwa watia moyo kwamba ukifanikiwa mmefanikiwa wote kama itakavyokuwa kwa wawindaji kwamba kila aliyeenda porini kuwinda hata kama mnyama aliyepatikana ni mdogo kila mtu aliyeshiriki hupata kidogo kidogo, ndivyo itakavyokuwa kwenu na kambi yako.kila mwanakamati inatakiwa kuwe na mtu anayemfuatilia ili kubaini ni yupi mpiganaji wa kweli na yupi mamluki, ,kwa sababu kuna baadhi ya wagombea hupandikiza masnitch kwenye kambi za wengine ili kupata taarifa za upande wa pili.mwanzoni unaweza kuwa na kambi kubwa mwishoni unabaki na kambi ndogo.epuka kuunda kambi mapema hii itasaidia kutofirisika mapema.

Ushauri wangu kwako tafuta fedha za kuwezesha kambi yako ya ushindi na si fedha za kuhonga wapiga kura, mpiga kura hahitaji fedha mpiga kura anahitaji goodwil .nakutakia ufanisi mwema katika kutekeleza ndoto yako
 
danya

danya

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Messages
3,164
Points
2,000
danya

danya

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2014
3,164 2,000
Kwanza kwa maelezo yako tu we we siasa huiwezi na wala haiko kwenye damu. Kama hata baba yako haijui siasa we we utapoteza hela zako bure. Siasa ni darasa refu lisilozoeleka so bora Fanya mambo mengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
usinikatishe Tamaa maana Sita kata tamaa kwa hili
 
danya

danya

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Messages
3,164
Points
2,000
danya

danya

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2014
3,164 2,000
Usikatishwe tamaa na coment za baadhi ya watu humu, tembea katika malengo yako. Kitu cha msingi ni kuanza kuwa jirani na wapiga kura wa eneo ambalo umechagua la kwenda kuwawakilisha wananchi wako., kikubwa kabisa kwenye siasa ni kuwa na goodwill na sio pesa nimesema hivyo kwa sababu umesema kipato chako ni cha chini mno. Tumeshuhudia matajiri wengi wenye pesa waliojaribu kuingia kwenye siasa walishindwa hii ni kutokana na kukosa goodwill.ukiwa na money + goodwill kazi yako inakuwa ndogo sana, ila ukiwa na fedha huna goodwil kufanikiwa kwenye siasa utachukua miaka mingi sana.ukiwa na goodwill huna fedha unaweza kushinda na kuwa mwakilishi mzuri

Hutakiwa kuwa na fedha nyingi sana za kuwapa wapiga kura, ila unahitaji kuwa na fedha za kuwawezesha wanakamati wako(kamati ya ushindi) kwa mafuta, stationary na posho, huku mara zote ukiwa watia moyo kwamba ukifanikiwa mmefanikiwa wote kama itakavyokuwa kwa wawindaji kwamba kila aliyeenda porini kuwinda hata kama mnyama aliyepatikana ni mdogo kila mtu aliyeshiriki hupata kidogo kidogo, ndivyo itakavyokuwa kwenu na kambi yako.kila mwanakamati inatakiwa kuwe na mtu anayemfuatilia ili kubaini ni yupi mpiganaji wa kweli na yupi mamluki, ,kwa sababu kuna baadhi ya wagombea hupandikiza masnitch kwenye kambi za wengine ili kupata taarifa za upande wa pili.mwanzoni unaweza kuwa na kambi kubwa mwishoni unabaki na kambi ndogo.epuka kuunda kambi mapema hii itasaidia kutofirisika mapema.

Ushauri wangu kwako tafuta fedha za kuwezesha kambi yako ya ushindi na si fedha za kuhonga wapiga kura, mpiga kura hahitaji fedha mpiga kura anahitaji goodwil .nakutakia ufanisi mwema katika kutekeleza ndoto yako
Nashukuru sana Sana
 
Forum statistics

Threads 1,284,199
Members 493,978
Posts 30,817,022
Top