Natamani nipate japo dakika………….!!!
‘Naamini alikuwa ndiye mwenye mapenzi ya kweli kwangu, nafsi inaniuma lakini sina jinsi`
`Alinifuatilia kwa muda mrefu sana nikajua ni mtu wa sound kama walivyo vijana wengine na pia sikuwa na mapenzi nae hata chembe.
Nakumbuka, siku ya mwisho aliponifuata nilimtukana sana aachane na mimi na akaamua kuondoka kwa hudhuni na kupanda piki piki yake na kuondoka. Kumbe masikini kaka wa watu alipata mawazo mengi hivyo kutokuwa makini barabarani, aligongwa na gari na kufariki dakika chache baada ya sekeseke hilo`
`Cha ajabu nilipopata taarifa za kifo chake niliumia sana na tangu hapo nimekuwa nikimuwaza sana na kutamani nipate japo dakika moja tu nimuombe msamaha kwa matusi niliyompa na mateso ninayoyapata juu yake!
Nasikitika sana mapenzi yangu kwake yamekuja baada ya yeye kwenda, nateseka sana juu yake na nakiri kuwa kumbe nilikuwa nampenda sana.`
Nimejikuta sihitaji mahusiano na mtu mwingine yeyote zaidi yake!
Nimemnukuu huyu binti ni rafiki yangu, anateseka serious na ameanza hata kunywa pombe!! Kifupi amekuwa kama kachanganyikiwa hivi, tumsaidie
ushauri jamani!!
Nawasilisha