Natamani News presenters wa Kenya wangekuja Tanzania

Stephen bryson

Senior Member
Oct 1, 2016
151
126
Mi nauliliza kwa nni kusiwe na exchange programme ya news presenter wa Tanzania na kenya, yaani tukampata Jeff koinange au Judy gichuru wakaja hapa bongo na wale wa bongo wakaenda kenya.
 
Tuko pamoja mkuu hawa jamaa wapo vzuri sana, kuna mmoja anaitwa hussein mohamed kesho anamhoji raila odinga saa tatu usiku, sikiliza maswali ya jamaa. Hvi wandishi wetu si wajifunze namna ya kuhoji na kuliza maswali.
 
Kuna haja ya waandishi wetu kuacha kufukuzia bahasha ila wajikite kwa maswali yenye tija sio zile leading questions zao! Pia njaaa ni mbaya sanaa
 
Wamiliki wa vyombo vya habari waweke exchange programme/ mikakati ya ushirikiano,

Mikakati hii itafanya waandishi wa bongo wawe wanaenda japo kwa miezi mitatu kenya,uganda,China,south Africa,ulaya au marekani,kutegemea na chombo kilipopata partner na ajenda ya chombo kwa kipindi hicho,may be kuongeza ujuzi kwa journalist wa uchumi,au siasa au michezo.

Nadhani pia vyombo hivi "havija-exploit" vya kutosha mashirikiano ya kikanda.

Kuna radio hurusha matangazo ya BBC,Sauti ya Ujerumani,Radio Japan,Radio France international,nadhani zinapaswa kuongeza kipengele cha mashirikiano kimafunzo.

Pia nadhani uandishi pia inahitaji kautundu kidogo,utafiti,kujisomea,kujua mazingira yanayokuzunguka ili unayemuhoji asije "kuku-trick" na facts
 
Sheria zenyu za vyombo vya habari ni mbovu kuzidi sheria za mkoloni!!!
Pambaufu kabisa.
 
Mi nauliliza kwa nni kusiwe na exchange programme ya news presenter wa Tanzania na kenya, yaani tukampata Jeff koinange au Judy gichuru wakaja hapa bongo na wale wa bongo wakaenda kenya.

Wanaweza kupotezwa ghafla.Ngoja tubaki na wanaokumbatia vyama
 
Shabani kissu,
Sie tuliua ustawi Wa jamii yetu, wakati kambarage anajenga ukomunist, na hapo ndio kila sekta ya ukuaji Wa maisha yatanzania yalipolemazwa, kuanzia elimu, siasa, Afya, miundombinu, haki sharia na vyote vinavyoendana kukua kama taifa, sasa ukianza kufananisha sisi na Kenya unakosea sana, Kenya na matatizo waliyonayo tangu Uhuru hawakuwahi kuchokonoa elimu yao na hakuna mwanasiasa anayejipenda anayethubutu kuchezea elimu, angalia sisi tangu Uhuru mabadiliko mangapi ya elimu yamefanyika na wewe msomaji ebu niambie lipi katika hayo mabadiliko yameleta tija? Tuache unafiki on a misuguano ktk mfumo Wa elimu yetu, watoto wa masikini wanasoma Kwa kiswahili kuanzia LA kwanza hadi LA saba, na watoto Wa matajiri wanasoma Kwa kiingeleza mpaka darasa LA saba, mwisho Wa Siku kidato cha kwanza hadi elimu ya juu wanakutana wote, wamasikini na matajiri sasa Kwa mtindo huu nani anaenda kufaidika? Tulidanganywa ujamaa sijui ukomunisti unaondoa matabaka badala yake hizi siasa poli ndio zimetuachia matabaka ya ajabu kwenye elimu na kuyaondoa ni gharama mno, namalizia Kwa kusema viongozi wengi Wa kiafrica waliozikumbatia hizi Sera za kijamaa au mie niite za kikomunist zilikuwa in Kwa faida zao Kwa ziliguarantee kukaa kwap madarakani muda mwingi kadri walivyopenda na wala si Kwa ustawi Wa jamii zao, kwani demokrasia, haikuwepo na Uhuru Wa vyombo vya habari ilikuwa hanasa na kama sisi tulifika mbali maana hata TV hatukuwa nayo, kama uongo naomba kukosolewa.
 
Samahani kwenye hoja yangu hapo juu nimeanza na jina LA shabani kissu kimakosa, naomba samahani kama nitaleta usumbifu wowote Kwa mhusika, kwani jina tajwa halihusiani na mchango wangu ktk mada.
 
Back
Top Bottom