Natamani kuwa mjasiriamali, nianze na Bodaboda au Taxi?

chameleon

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
555
170
Wanajf wenzangu naomba ushauri wenu muhimu ili wasijesema nimeuingia mji kwa pupa. Binafsi nimepata mkopo wa Tsh milioni 10 toka kwa mfadhili wangu. Utafiti wa haraka haraka nilioufanya nabaini kuwa kwa pesa hiyo naweza kumiliki pikipiki za Mchina 6 ingawa nitaonekana lofa lakini nitaajiri malofa wenzangu 6 na sitatozwa kodi au ninuegari saloon 1(used) nikaheshimika na serikali ambayo itanitoza ada (tax cab), road licence pamoja na kodi yamapato.
Naombeni ushauri tafadhali.
 
Fanya berbershop ya viti viwili vya kunyoa,kimoja cha scrub na kimoja cha kuonyeshea,itatosha hyo 10M.ukipatia mtaa mzuri kwa kiwango hcho cha berbershop hyo utaweza ingiza kiasi kisichoshuka laki1 per day..ukisema ununue gari ufanye taxi hakikisha unaendesha mwenyewe ndo utarudisha hyo pesa kwa wakati,ukimpa dreva kumbuka atakupa elfu80 au 70 per week,utakaa na mkopo wa watu kwa muda mrefu na kuingia kwenye lawama,yote kwa yote endesha jambo unaloona ndo unapenda kulifanya
 
Hongera sana Kinyonga kwa wazo zuri la biashara, nadhani kuliko kufanya biashara ya taxi ni bora ununue bodaboda maana turnover itakuwa kubwa kuliko Taxi 1. Bodaboda moja kwa wiki ni tu-assume sh.40000x6=240000 kwa wiki ambapo kwa mwezi itakuwa hivi 240000?4=960000 kwa MWAKA 11520000. Baada ya miaka 2 utakuwa na 23040000. Baada ya hii miaka miwili unaweza kuuza hizo bodaboda maana zitakuwa zimeanza kuchoka.
 
Wanajf wenzangu naomba ushauri wenu muhimu ili wasijesema nimeuingia mji kwa pupa. Binafsi nimepata mkopo wa Tsh milioni 10 toka kwa mfadhili wangu. Utafiti wa haraka haraka nilioufanya nabaini kuwa kwa pesa hiyo naweza kumiliki pikipiki za Mchina 6 ingawa nitaonekana lofa lakini nitaajiri malofa wenzangu 6 na sitatozwa kodi au ninuegari saloon 1(used) nikaheshimika na serikali ambayo itanitoza ada (tax cab), road licence pamoja na kodi yamapato.
Naombeni ushauri tafadhali.

Ila hakikisha unaajiri watu wanaojitambua. Sifa awe na mke na watoto
 
Hongera sana Kinyonga kwa wazo zuri la biashara, nadhani kuliko kufanya biashara ya taxi ni bora ununue bodaboda maana turnover itakuwa kubwa kuliko Taxi 1. Bodaboda moja kwa wiki ni tu-assume sh.40000x6=240000 kwa wiki ambapo kwa mwezi itakuwa hivi 240000?4=960000 kwa MWAKA 11520000. Baada ya miaka 2 utakuwa na 23040000. Baada ya hii miaka miwili unaweza kuuza hizo bodaboda maana zitakuwa zimeanza kuchoka.

Asante kwa ushauri mzuri mkuu nitaufanyia kazi.
 
Hongera sana Kinyonga kwa wazo zuri la biashara, nadhani kuliko kufanya biashara ya taxi ni bora ununue bodaboda maana turnover itakuwa kubwa kuliko Taxi 1. Bodaboda moja kwa wiki ni tu-assume sh.40000x6=240000 kwa wiki ambapo kwa mwezi itakuwa hivi 240000?4=960000 kwa MWAKA 11520000. Baada ya miaka 2 utakuwa na 23040000. Baada ya hii miaka miwili unaweza kuuza hizo bodaboda maana zitakuwa zimeanza kuchoka.

Toa elfu 15000 ya service kwa kila bodaboda kwa kila wiki then uweke figure nyingine hapo.
 
Hongera sana Kinyonga kwa wazo zuri la biashara, nadhani kuliko kufanya biashara ya taxi ni bora ununue bodaboda maana turnover itakuwa kubwa kuliko Taxi 1. Bodaboda moja kwa wiki ni tu-assume sh.40000x6=240000 kwa wiki ambapo kwa mwezi itakuwa hivi 240000?4=960000 kwa MWAKA 11520000. Baada ya miaka 2 utakuwa na 23040000. Baada ya hii miaka miwili unaweza kuuza hizo bodaboda maana zitakuwa zimeanza kuchoka.
Umempa ushauri mzuri,ila mie nijuavyo na kama mdau wa bodaboda ni kwamba hesabu ni 50,000 kwa wiki kwa upande wangu,sijui maeneo mengine,na ni mkataba wa mali kuendelea kuwa yangu.

Halafu ukweli ni kwamba 10 hawezi kununua bodaboda 6 hata siku moja.Huu utani.
Sasa 10m asiipe ndoto kubwa.
Itambulike kwamba Drivers wa bodaboda kwa sasa wanachagua pikipiki za kuendesha,ukinunua vimeo hakuna atakaetaka kundesha pikipiki zenye majina ya ajabu,na matatizo ya kila mara.Abiria wenye pia wanachagua pikipiki za kupanda.

Sasa kabla hajanunua,atafute kwanza drivers na kila driver amuulize anataka pikipiki ipi,then ndio anunue.Ila kama akienda kununua kwa kuona kwamba kila driver ananjaa,basi atabadilisha kila siku drivers.

Mie hutumia style ya kumuita driver na kwenda nae dukani aseme mpaka rangi anayoitaka,wapo waliochukua Boxers ambao ndio wengi nilioanza nao na wangeni walitaka SUnlg.

Sasa hapa lazima umakini uwepo pia.

Kwa hesabu ya 10m,hapo huja ujanja wa kununua bodaboda zaidi ya nne.
Kuan Bima na vibali,na kuna pesa ya mwanasheria wako.So akikuambia mtu unapata hata tano basi jaribu uone then utanipa matokeo yake.
 
Ushauri:
Kwa kuwa ni mgeni kwenye biashara hii ya vyombo vya moto.Basi usiwekeze pesa yote kwenye biashara.
Hao unaowaona wenye bodaboda mpaka 50,jua walianza na moja au mbili,na hao wenye Mabasi 10 walianza na moja au mawili.
Kwa changamoto za biashara hii,lazima uwe stable sana,ukianza kwa pamoja itakuvuga sana,hakuna pesa nyepesi kwenye kuhangaika,so lazima upambane na changamoto.
Kama ni bodaboda basi nunua mbili tuuu,then pesa inayobakia weka bank,kisha baada ya miezi mitatu ndio ongeza tena,hapo ndani ya miezi mitatu utakuwa umeishaanza kuona mwanga wa biashara na kupambana kwake.
Kuna watu walinunua bodaboda wiki ya mwanzo na mwezi ujao wakauza,hawa nawaita watoto wa Mama yao nepi.Wanafikiria kila kitu rahisi.

Muono wangu wa pili:
Nunua Bajaji moja,then na bodaboda moja.
Hii ni biashara moja,inachangamoto kadha zinafanana,ila zipo changamoto kubwa hazifanani.Hapa utasoma kitu.
 
Nunua boda boda mbili tu. Moja endesha mwenyewe nyingine mpe dreva. Hela inayobakia kanunue shamba uanzishe kilimo chochote. Siku za jumamosi utaenda shamba na pikipiki yako upige kazi. Fedha unazopata kwenye biashara zitasaidia pia huko shamba. Soon utakuwa na mtaji mkubwa sbb shamba litaongezeka thamanu muda mfupi tu. Unaweza hata kuweka kibanda uko ukaweka mifugo midogomidogo
 
Kuna watu walinunua bodaboda wiki ya mwanzo na mwezi ujao wakauza,hawa nawaita watoto wa Mama yao nepi.Wanafikiria kila kitu rahisi.

Ha aha ha ha, hapa mkuu umegusa kwenye mboni yangu, kuna kijana nimempa boda boda tena ya mkataba huu mwezi wa pili sasa, hadi sasa namdai mapato ya wiki mbili maana analipa kila mwisho wa wiki, mwenyewe anasema atajipanga na kufidia hilo gap, usipokuwa na roho ngumu unaweza kupata wazo la kuuza.
 
Back
Top Bottom