VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Mara kwa mara Rais Dr. John Pombe Magufuli amekuwa akisema, katika hotuba zake kimasikitiko, kuhusu uwepo wa wafanyakazi hewa, wanafunzi hewa, kaya hewa na hata mishahara hewa. Rais amekuwa akiyasema maneno haya katika namna ya kuyarudia ili kuonesha kuwa alipoingia madarakani, alikuwa na kazi kubwa ya kusafisha 'nyumba' yake.
Yaani, Rais alikuwa akiweka mambo sawa kwa kuziba mianya na mapengo yote ya kifisadi. Ni dhahiri kuwa wafanyakazi hewa,wanafunzi hewa, mishahara hewa na hata kaya hewa zina mwanzilishi wake. Hizi zina aliyezisababisha. Sibishi kuwa ni maumivu makubwa kinchi kuwa na vitu na watu hewa wanaolipwa kwa kodi ya wananchi wanyonge wa Tanzania.
Natamani sana kukubaliana na Rais kuhusu uwepo wa watu na vitu hewa na umuhimu wa kupambana na mambo hayo. Lakini, kuna jambo moja linanitatiza. Wako wapi waliosababisha mambo hayo? Wanapelekwa mahakamani lini ili nasi tuwaone kwa uchungu waliosababisha 'u-hewa' huo kila mahali?
Watakapofikishwa mahakamani wahusika wa mambo yote hewa-hasa la watumishi na mishahara hewa, nitakubaliana na Rais katika mapambano haya. Shime Rais, amuru wahusika waburuzwe mahakamani.
Mwafaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam