Mimi nami nilipenda sana Mke wangu tupate mapacha. Mzao wa kwanza tukapata mapacha 4 (sijui wanaitwaje, manake mapacha ni wawili, wakiwa wanne sijui), wakiume 3 na binti 1. Ila ilitokea tu hakukutumika dawa yoyote. Wakati wakiwa wachanga ilikuwa kazi kuwalea, ilibidi kweli nisitishe shughuli zangu zote nilizokuwa nafanya kumsaidia mamaa kulea. Lakini sasa wamekua kiasi raha sana ukiwaona.