Nataka kumsahau huyu mwanamke, nifanyeje?

MUGUNDA

Member
Aug 11, 2011
69
62
Jamani wana JamiiiForums,

Niliweka post hapa mke wangu alivyoondoka na akaenda kuishi kwake yaani chumba cha kupanga.

Ila ninakaa namfikiria kila mara hasa kwa mabaya aliyonifanyia, hii hali inanitesa sana, nakaa nikiwa mtu wa hasira na huwa napata usingizi,nikienda bar angalau nikanywa bia kama nne hivi kwa siku.

Nataka kumsahau huyu mwanamke na nimuone kama mtu wa kimataifa je nitumie njia gani? Kaniachia mtoto mmoja naye kaondoka na mtoto mmoja.

Nawasilisha.
 
Usijisumbue saana kufikiria kutoa mawazo yake maana kadri unavyofikiria hvyo ndo unazidi kujiumiza
We ishi maisha2 maumivu yakija yaunganishe na mabaya aliyokutendea apo kaz itaisha
 
Waza tu utadouble Vipi asset Zako! Jiwekee malengo ya wiki, mwezi, Miezi 3, 6 mpaka Mwaka! Yaani kila siku iwe Na Impact Ktk malengo yako! Hapo utamsahau faster.
 
Hamishia mapenzi na mawazo yako kwa watoto wako, Toa vitu vinavyokufanya umkumbuke, Usijilaumu kwa kilichotokea fikria mbele kwa mbele, tafuta mtu unaye mwamini umweleze jinsi unavyojisikia na utapata ushaur ama hata hapa JF, Usimpigie simu kabisa.
 
Huwezi kumsahau kwa sababu mna watoto pamoja

Invest kwa watoto wako and desire to see them become successful

Use the pain you feel as a drive

Punguza hasira chagua kusamehe kwa moyo mkunjufu, keeping hating unajiumiza mwenyewe
 
Sijui alio kufanyia lakini lakwanza jaribu kumsamehe na uone kua hakuna asie kosea as long as ni binadamu,na usiangalie makosa aliokufanyia wewe tuu jiulize ndani ya nafsi yako je hujawahi kumkosea iwe dhahiri au kwa siri?
Kua na moyo wakiume na let it go,kila binadamu ana mazuri yake na mabaya yake usisahu mazuri yako japo moja
lakini kumbuka na fanya ndio sababu yakumsamehe,SALI kwa sana pinshallah mwenyezi mungu atakupa upole wa nafsi...
 
Ndugu bado una mapenzi nae.... jaribuni kisuluhisha.... for better.
 
Bora umeachiwa mmoja nimeachiwa watatu nachofanya napiga sana mzigo madogo wanaenda shule fresh maji kimtindo muvi kwa sana nikiwa home maisha yana songa na kichwani hayupo kabisa.
 
Binafsi nitaongea generally sababu sijui kwanini mmeachana ama kwanini amehama....

Ili umsahau jaribu kukubali ukweli kwa njia za kimatendo sababu ni kweli hayupo na kumkumbuka inaku umiza weye zaidi shekhe wangu.

1. Jipatie muda ukiwa peke yako haufanyi kitu chochote kwa angalau lisaa moja ( kils siku, jijengee tabis hiyo pia, inasaidia kukupatia suluhisho sahihi na maamuzi mazuri na kujiamini mkuu)

2. Ukiwa peke yako lazima mawazo yake na mengine mengine yatakujia,
Tumia muda huu kujifunza kukemea vitu ambavyo hauvitaki sababu havina manufaa kwako....

Kukemea na maanisha kila wazo ama hisia ama chochote kikujia tamka kwa kukemea mfano
" ondoka, toka, get off, stupid, crazy taja jina lake, yaani pambana si lazima yawe maneno machafu unaeza sema hata God Forbid, yaani kama ni kitu disgusting hautaki kiona.

Kama vile ukiona kitu mbaya unavyosisimka na kutaka ku quit.

Usinye pombe, wala kutumia chochote kilevi coz hauta escape bali utafanya mambo ambayo yatampeleka mbali zaidi coz she already faded up.

Kila la heri mkuu.

Mfano kama mimi ni wewe na amekimbia kwasababu ameona simfai na sababu kubwa huwa ni pressure kutoka kwa jamaa mwingine then bro never get back to her ukimsahau hata kama atahitaji msaada wako just help her end...

Weka ukutuka mkubwa maana huyo ni blood sucker mahfakaha!

Knowthyself
 
Muda huponya yote.Hamna dawa we jikaze mwanaume.

Ila nasikia uchungu nikiona mwanaume mwenzangu anasononeka kwa sbb ya ke.

Kadiri siku zinavyoendelea mwanamke anazidi kutukuka na kuman-up lakini vijana wa kiume wakisurrender na kunyenyekea,kulialia.Manung'uniko hayaishi.Jikaze tafuta mwingine.Jiamini.
 
Back
Top Bottom