Nindoto yangu kugombeya ubunge maishani mwangu,kwasasa nasomea ualimu, mwaka wa mwisho,namaanisha 3rd yr kuanzia october 8, nawaza. na natamani sana kuwa mkombozi na mtetezi wa wanyonge maisha yangu yote ila tatizo sijui nitaanzia wapi ili kutimiza ndoto hii.Wadau,wanasiasa nisaidieni mawazo hapa niko sirious kugombeya ubunge katika jimbo moja hapa Tz je niwapi pakuanzia,
Kwanza itabidi niwe na pesa kiasi gani ili nigombee huo ubunge?
kutokana na fani nayo isomea na jun mwakani natumaini nitakuwa nime maliza je nitakuwa sahihi kugombeya?
Je ninini chauongeza au kujiandaa kielimu kiuchumi ama kisisiasa ili niwe kamili.
Mheshimiwa mtarajiwa,
Ili kuwa Mbunge kuna mengi sana ya kujifunza... kwanza lazima ufahamu Mbunge ni mwanasiasa na hakuna chuo chochote kinachotoa elimu ya Ubunge. Kwa kuanzia unaweza kufanya haya yafuatayo:
1. Anza sasa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi hapo chuoni kwako anzia mwakilishi wa darasa hadi uraisi wa chuo..hii inategemeana na muda wako hapo chuoni
2. Jichanganye hata kwenye mambo ambayo huyapendelei.. sehemu za kijamii...kugombea nafasi mbalimbali za uongozi popote upatapo nafasi kuanzia mwenyekiti wa kamati za maandalizi ya sherehe za kijamii hadi kwenye vilabu mbalimbali vya michezo... jipitishepitishe kwenye vilabu/ Baa toa ofa za vinywaji watu wakujue..kumbuka siasa haina dini.
3. Jifunze kutokuwa na misimamo wala kutunza kumbukumbu za nyuma yaani kama leo uko CCM ukasema CDM ni wachawi halafu ukakosa nafasi ya kugombea ndani ya CCM kisha ukaamua kuhamia CDM basi usisite kusema CCM ni wanga.
4. Jitolee kufanya kazi mbalimbali za kijamii... hamasisha utunzaji wa mazingira eneo ulilopo..hamiasisha watu wapande miti, walinde vyanzo maji nk. pia kuwa mbele kwenye shughuli zote za kutetea haki..kama maandamano nk.... usiogope virungu vya polisi.
5. Angalia mapungufu ya kiongozi ambaye unataka kuchukua nafasi yake jaribu kuwaeleza watu mapungufu hayo na vipi unadhani unaweza kutoa suluhisho......
6. Jitunze pia ujiheshimu hasa ukiwa kwenye mwanga..na njia pekee ya kujionyesha hivyo ni kwenda kwenye nyumba ya ibada...chagua kukaa sehemu ya mbele kabisa..lakini usijitambulishe nje ya nyumba kuwa wewe ni dhehebu gani.
7 Jifunze kuwa na ustahimilivu na usiwe na jazba yaani kama umetukanwa basi usirushe ngumi wala kwenda kufungua mashtaka isipo kuwa na wewe unatakiwa ujibu mapigo kwa kutukana....hayo ndiyo maisha ya kila siku ya mwanasiasa.
Mheshimiwa mtarajiwa..... kama una nia ya kweli kwamba unataka kuwatetea wanyonge na si tamaa ya marupurupu wanayopata wanasiasa au nafasi ya kufanya ufisadi...anza kuwatetea kwa nafasi utakayo kuwa nayo ya ualimu....wafundishe vijana wetu waelewe jitolee muda wako wa ziada waelimishe wale wazito kuelewa hapo utakuwa. umewatetea kiasi cha kutosha.
Kama ni mchamungu basi nakushauri ubaki kwenye kazi yako..... kwani kazi ya ualimu ni kazi ambayo rahisi kwenda peponi/Mbinguni kuliko kazi ya siasa ambayo kila siku unajilimbikizia dhambi na mwisho wake unaishia motoni.
..........yapo mengi sana.........tena sana