Nataka kufanya biashara ya maua (fresh flowers) toka Arusha

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,296
15,583
Heshima wakuu. Mi nimtumishi ila pia ni mjasiliamali, pamoja na mambo mengine ninayofanya nimefikiria kufanya biashara ya fresh flowers kutoka Arusha kwa ajili ya kupamba maofisini na pia kutengeneza mataji kwa shughuli mbalimbali. Wazo hili nililipata siku nimetembelea pale Namanga Dar nakujionea jinsi biashara hii inavyoonekana kuwa kubwa na yenye fursa kwa bahati mbaya sikupata muda wa kuongea na wahusika kujua zaidi ila nilisikia tu kwamba maua yanatoka Arusha.

Sasa basi naomba kwa yeyote anaejua upatikanaji wa maua haya Arusha tupeane ushauri na uzoefu maana huku nilipo hakuna mtu anaesupply fresh flowers maofisini na nimeongea na baadhi ya makampuni wameonesha interest na kuniambia nipeleke proposal. Sasa kabla ya kupeleka prososal naomba msaada wa ushauri zaidi wakuu.
 
Back
Top Bottom