Natafuta wanunuzi wa mayai

Hayana utofauti na kuku wa kienyeji.
Biashara nzuri hii ngoja waje
 
Punguza bei hiyo mkuu ni kubwa sana labda kama unataka kuwauzia watu wa huko Kigamboni maana wa mbali akiingiza na usafiri ni loss kwake mfano muuza duka kwa hiyo bei labda auze kwa jero ambayo itakuwa hasara kwake maana yai sasa hivi ni 400 na akiuza 400 ni hasara pia maana faida yake ya buku itakuwa imetumika kwenye usafiri.

Bei ya sasa ni 9000 - 9500.
 

Sasa mbona simu haipo hewani tufanye biashara?Kuku nao unao
 
Wa mbali unaletewa usafir upo, pia haya mayai huuzi kama ya kisasa, utauza kwa bei ya mayi ya kienyeji lakini kwa bei pungufu kidogo.
Karbu tukuhudumie.
 


Hongera mkuu kwa biashara. Nadhani wahitaji watakutafuta. Lakini swali langu ni moja " je mayai yenye kiini cha njano ni asili yao au ni aina ya chakula/virutubisho wanavyokula" Au mkuu unawalisha nini ili kupata kiini cha njano!


Asante
 
Wa mbali unaletewa usafir upo, pia haya mayai huuzi kama ya kisasa, utauza kwa bei ya mayi ya kienyeji lakini kwa bei pungufu kidogo.
Karbu tukuhudumie.
Sawa mkuu

Hebu picha tuone ukubwa wake kama hutojali
 
Hongera mkuu kwa biashara. Nadhani wahitaji watakutafuta. Lakini swali langu ni moja " je mayai yenye kiini cha njano ni asili yao au ni aina ya chakula/virutubisho wanavyokula" Au mkuu unawalisha nini ili kupata kiini cha njano!


Asante
Hawa kuku nimefuga kitalamu, wanatumia vyakula asili na nyasi. Ukihitaji ntakupa maelekezo ya kutosha.
 
Mayai chotara
 
Duuuu trei _450 per day!
Hongera Mkuu kwa kufuga
 
Reactions: amu
450*11,000=4,950,000 per day. Thats good business. Tafuta sales person.
 
sijui nasema vibaya lakini huu ni ushauri wangu!
dodoma kwa sasa mayai yamepungua sana "tunapata tabu sana" tray limefika shillingi 10,000/- hivyo kama ukiweza kuyaleta kwa bei ya jumla mpaka yanafika ikawa 9000/- unaweza kuwa na wateja wazuri. piga hesabu zako kama inalipa jipange kuuza kipindi hiki cha baridi kuna soko zuri kwa kuwa utagaji umeshuka.
 
Mfugaji mwenye kuku 13000+ ila hajui soko wala bei ya jumla na reja reja......

Reja reja ndio 11000
Jumla ni 9000-9500

Mzigo mkubwa huo ukiupunguza bei unaisha mapema.

Ukibakia na bei yako hiyo utayala mwenyewe
 
Kuna Bakery zinatumia Trey 70 kwa siku zungukia Bakery sema wanalipa baada ya wiki 2
 
Reactions: amu
Hayo huwezi kuuza kama ya kienyeji,kwakuwa rangi ya gamba la juu ni sawa na ya kisasa,kumwambia mteja anunue kwa 500 kwakuwa tu kiini ni cha njano,mteja hataamini,
kwa ushauri tu fanya bei ya jumla 8500 uingize hela faster faster,
kama itakulipa lakini,
bei ya mwisho wa madukani uzia 10500 kama kweli yana ukubwa wa kuridhisha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…