Natafuta uongo wa kumwambia mke wangu ila nimekwama

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,519
22,011
Mke wangu alichukua simu yangu na kufuta namba ya mpenzi wangu Naomi kisha akahifadhi namba yake kama Naomi. Sikujua kuwa kuna mtu alimwambia mke wangu kuhusu Naomi.

Nilipokea SMS kutoka kwa Naomi akiomba pesa kiasi cha 2,000,000/= sikuwa na hiyo hela hivyo nilimkimbilia mke wangu na kumdanganya kuwa nahitaji 2,000,000/= kwa dharura. Nilimwambia kuwa kaka yangu anaumwa na anahitaji pesa haraka.

Mke wangu alinipa zile pesa na nikakimbilia kutuma kwenye akaunti namba iliyoandikwa kwenye ule ujumbe nikijua kuwa ni Naomi. Nikiwa nimejipumzisha nyumbani baada ya kutoka kazini, niliendelea kuwaza iwapo Naomi alipokea pesa hizo maana hakuwa amenipa mrejesho kama amepokea ua lah.

Nilimtumia SMS ili kujua kama alikuwa amepokea pesa. Jibu lake lilikuwa, "Nipigie sasa." Nilitoka nje nyuma ya nyumba kupiga simu na simu ilipopokelewa hapo ndipo nikajua za mwizi ni siku 39 tu ikifika ya 40 anatiwa ndani.

Nilisikia sauti ya mke wangu badala ya Naomi akiniambia "njoo huku ndani nikupe jibu lako"

Yamepita masaa matatu bado nimesimama nje ya nyumba na mvua inakaribia kunyesha. Sijui jinsi ya kurudi nyumbani kwangu.

Ushauri wowote tafadhali!
 
1671751327922.png
 
Back
Top Bottom