Natafuta soko la Mayai ya Kienyeji

Pretty P

Senior Member
Dec 27, 2010
121
20
Wapendwa habarini, Natafuta soko la mayai ya Kuku wa kienyeji nina sambaza kwa wenyeji wa Dar.
 
Kuna hili tangazo nililiona IG hebu pitia uone kama litakufaa
9ff867bca394e61152bd50c39fe9ca5b.jpg
 
Mkuu inaonekana haupo serious na biashara. Kama wewe ni mfugaji wa kuku wa kienyeji na una uhakika wa kutoa tray kadhaa za mayai kila siku huwezi komaa na hiyo bei ya elfu 15 kwa tray , na delivery sh. 2000/- hivyo total ni elfu kumi na saba.....it can't be , and seems you're joking!

Ni lazima ujue kujenga network hasa ukiwa mfugaji na hiyo itasaidia kuwa na soko la uhakika. Let say unauza tray 5 kila siku @12,000/= kwa muda wa wiki = 5 x 12,000/= x siku 7 = 420,000 x 4 weeks = 1, 680,000/=. Hapo huna hasara jombaaa!

Lakini wewe inaonekana haupo serious na hiyo biashara au unafanya biashara kimazoea tu na sio kwa maana ya kutaka kuwa na faida endelevu.

Kifupi nakupa pole. Huwezi tajirika kwa namna hiyo hata siku moja ndugu.

Huo ni ushauri wa bureee hutaki....unaacha tu.
 
Mayai ya kienyeji uchafu mtupu, mengine unakuta yametamiwa, mengine machanga, mengine viza, na vingine vidunchu nashindwa kuelewa kinachofanya yauzwe ghali nini wakati nutrition yake ni poor kuliko mayai ya kisasa
Kumbe nutrition ni maganda na ukubwa wa yai siku hizi. Unajielewa kweli mkuu
Ukisikia mayai ya kisasa ni ya kisasa kweli yaani unakula kemikali tupu mkuu lakini ukisikia mayai ya kienyeji ni kienyeji yaani ni natural tupu mkuu.
 
Kumbe nutrition ni maganda na ukubwa wa yai siku hizi. Unajielewa kweli mkuu
Ukisikia mayai ya kisasa ni ya kisasa kweli yaani unakula kemikali tupu mkuu lakini ukisikia mayai ya kienyeji ni kienyeji yaani ni natural tupu mkuu.
Wewe ndo hujislewi. Mimi nafuga kuku wa kienyeji na wa kisasa na wote nawapa vyakula vya viwandani sasa wewe umejikaririsha kuwa kuku wa kienyeji wanaproduce mayai natural. Alafu pia sujui kinachokufanya useme mayai ya kisasa ni kemikali tupu, huo utafiti umeufanyia wapi
 
Mayai ya kienyeji uchafu mtupu, mengine unakuta yametamiwa, mengine machanga, mengine viza, na vingine vidunchu nashindwa kuelewa kinachofanya yauzwe ghali nini wakati nutrition yake ni poor kuliko mayai ya kisasa
Ukipewa ushauri na doctor ule mayai wala hautoambiwa kula mayai..utaambiwa kula mayai ya kienyeji.. ukubwa wa yai la kisasa wala haifikii hata robo ya kipande tu cha yai la kienyeji..kukuta mayi viza ni uhuni tu wa wauzaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana jamiiforum na wasomaji wote wa habari za matangazo madogodogo. Mi naitwa DEOGRACIUS JOSHUA ,Ama waweza niita DEO MAYAI. Nipo ninapatikana jijini dodoma sehemu chamwino, ni mjasiriamali wa kuuza mayai ya kienyeji pamoja na kuku wa kienyeji.
.
MAYAI YA KIENYEJI
ninatafuta soko la mayai kwa mikoani na hata Dodoma pia, kwa watu wa majumbani sokoni madukani na kila sehemu yenye uhitaji nayo panapo uhitaji tutafanya biashara. Bei ni Tsh. 12,000/= kwa trey moja kwa wakazi wa Dodoma, na Tsh. 13,000/= kwa wateja wa mikoani. Usafirishaji ni juu yangu.
Mawasiliano yangu ni 0685564008 na 0659825820
.
.
KUKU WA KIENYEJI
Pia ninauza KUKU wa kienyeji pekee kwa bei ya Tsh. 13,000/= na Tsh. 14,000 kutokana na ukubwa ndo mana bei zimetofautiana .
Mawasiliano namba 0685564008 na 0659825820
.
.
MAYAI VIZA
Katika kuuza mayai pia kwa wale wanaokuwa na uhitaji wa mayai visa pia yanapatikana bei ni Tsh. 1,000/= kwa kila yai viza moja. Usafirishaji ni juu yangu.

Mawasiliano moja kwa moja kwangu
DEO MAYAI
0685564008
0659825820
Chamwino dodoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom