Natafuta smartphone ya kununua

TO2004

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
540
Reaction score
220
Wakuu nahitaji smartphone yenye sifa zifuatazo- iwe ni Android,,Flash,Touch screen. Budget yangu ni 150000 Kama unayo ni pm tufanye biashara,Nipo Dsm NOTE:Huwawei Y300 siitaji
 
Nina Nokia24... kama upo tayari ni pm
 
Nenda shop utapata tecno android kwa 15k
 
Wakuu nahitaji smartphone yenye sifa zifuatazo- iwe ni Android,,Flash,Touch screen. Budget yangu ni 150000 Kama unayo ni pm tufanye biashara,Nipo Dsm NOTE:Huwawei Y300 siitaji

Mkuu kwa pesa hiyo na uko Dsm. Halafu unataka simu za mkononi !!!. Ingawa siku Tz, alkini ngoja nikupe dili: Ongeza 10,000/=, nenda Posta mpya, maduka yaliyopo jirani na askari monument - duka la pili kutokea kutokea Benki ya Posta utapata Tech H 5 au P5; watakuanzia 250,000/= au 220,000/=, komaa sema una 150,000/= watashuka mpaka 180,000/= sasa mwenyewe utajua cha kufanya. Ukishindwa, ni-pm nikuelekeze kwa mtu ukachukue Tecno H 5 kwa 150,000/- ameinunua kipindi cha 7,7,.
 
nimepapenda hapa!!!,hata mie sina imani na simu za kununua mkononi

Inategemea umenunua ipo katika hali gan. Na aliye kuuzia ni mstaarabu au kakupiga changa la macho..Watu kibao wanatumia simu used na zipo poa. Sio kila mtu ana huwezo wa kununua simu dukani..
 
Kabla ya kununua simu hizo za Android,Flash,Touch screen kutoka mkononi mwa mtu, zingatia ushauri wa polisi hapo chini:

TAARIFA MUHIMU KUTOKA JESHI LA POLISI NCHINI:

JESHI LA POLISI NCHINI LINAPENDA KUKUJULISHA MTANZANIA KUWA, KWA USALAMA WA MAISHA YAKO:-

1. Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.

2. Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.

3. Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina sh ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako inahusishwa na tukio hilo.

4. Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.

5. Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali. Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhumiwa namba moja. Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.

MPE ONYO NA MWENZAKO.
 
ndroid,,Flash,Touch screen, HIZO SIMU UNAZOSEMA ZINA SIFA ZOTE HAPO?
 
Wakuu nahitaji smartphone yenye sifa zifuatazo- iwe ni Android,,Flash,Touch screen. Budget yangu ni 150000 Kama unayo ni pm tufanye biashara,Nipo Dsm NOTE:Huwawei Y300 siitaji

Segerea hiyo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…