Natafuta simu ya Oneplus 5T

Natafuta simu ya Oneplus 5T

mi_mdau

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
1,171
Reaction score
1,757
Habari wakuu
Natafuta simu ya Oneplus 5T hapa bongo, kuna mtu anajua inaweza kupatikana wapi? Wauzaji wwngi hawana hii
 
Ngoja ni_subscribe hapa..Hii simu ni nzuri ila sijui kama Bongo imefika
 
ipo kuna mtu anayo labda bei ndo tatizo
 
Tafuta online, kwa bongo si rahisi kuzipata. Hata ukipata ni kwa bei kubwa...
1140a8951bdb8f97c10ee9c85735aa7d.jpg

Asante ila online mpaka ifike ni shughuli na naogopa uncertainties za kodi na shipping fees. bei hii ya 5T ni kama aliyokuwa anauza huyu jamaa wa hapa bongo. Labda nimsubirie kama atazileta tena. Ukiwa na mtu marekani ni rahisi kidogo unaipata kwa dola 500 tu
 
Asante ila online mpaka ifike ni shughuli na naogopa uncertainties za kodi na shipping fees. bei hii ya 5T ni kama aliyokuwa anauza huyu jamaa wa hapa bongo. Labda nimsubirie kama atazileta tena. Ukiwa na mtu marekani ni rahisi kidogo unaipata kwa dola 500 tu
acha woga mkuu, mtafute MwlRcT yuko humu jf hasa kule kwenye forum ya matangazo anakuagizia na anakufikishia hadi ulipo.
 
Tafuta Xiaomi MI 5, MI 6, au MI Mix2 maana ndio mshindani mkubwa wa honor, oneplus na oppo ktk soko la smartphone China kwa sasa
abe1b6f226bbb612a52a31be83a3a6a7.jpg
901441a7cb905ef4882cc7292038dc4d.jpg
8f6c6e2351fa79d4d2c9de48de886896.jpg

Asante ila oneplus wako vizuri zaidi hasa kwenye Software na updates
 
Agiza mkuu, Mimi natumia 3T na nzuri Sana. Wakati wa kuagiza zingatia sub model iwe ya Europe/Asia ndio LTE karibu zote za hapa mjini zinashika. China model unapata LTE ya Zantel na north America hamna kabisa 4G(Labda ambayo Sifahamu) though 3G zote utazipata kwenye zote. Pia usiitumie ilhali haina screen protector, Digitizer yake msala.
 
Mkuu nenda City Mall, ukiingia tu langoni duka la pili mkono wa kulia wanzano 3, 3T, 5 na 5T.
Asante mkuu pale nilipita wanazo 5 na 5T. Bei zao zimechangamka ila nawaelewa kwa sababu ya kusafirisha, kodi ya duka, kodi ya mzee mkubwa n.k. ila wanakupa warranty na receipt.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom