Natafuta sehemu ya kujitolea, kazi au shughuli yeyote ya kunipa experience

soshoMidia

Member
Nov 11, 2020
70
62
Habari zenu ndugu zangu,

Mimi ni graduate nina shahada ya teknolojia habari na mawasiliano (IT) jinsia mwanaume, umri miaka 25 nipo Dar es Salaam nina uzoefu katika networking and computer maintenance pia ni fresh from university mwaka wa masomo 2019/2020.

Baada ya kukaa mtaani kwa muda na kusambaza CV zangu hapa na pale bila kupata majibu nimejipata hali hii inanipa wakati mugumu nini cha kufanya mana muda nao unakwenda kasi nikijiangalia naona kama nipo nyuma.

Hivo basi, nimechukua uamuzi wa kuja huku kwenye hii familia kuomba kwa yeyote mwenye uhitaji na mtu mwenye kariba yangu anisaidie japo sehemu ya kujishikiza huku nikipata experience au hata kazi moja kwa moja kama ikitokea.

Pia kazi yeyote unayofundishika kwa muda mfupi naweza fanya mana nipo mwepesi kwenye uelewa.

Naimudu excel pia katika fani yangu hivo natanguliza shukrani kwenu.

Asante.

Mawasiliano: 0787357219
 
mana muda nao unakwenda kasi nikijiangalia naona kama nipo nyuma.
Hii presha isitawale sana akili yako ukajikuta unafanya mambo mabaya au maamuzi yasiyo mazuri,kuna watu tuko nao kitaa tena wanaume wana miaka 36+ na mpaka sasa hawana direction,take a breath na utulize kichwa katika kutafuta nini cha kufanya, ukijiona uko nyuma sana kwa umri wako usije angukia mikononi mwa kina GINIAMBI tukakukosa ukiwa bado ni nguvu kazi..muhimu MTANGULIZE MUNGU MBELE KWA KILA JAMBO.

Dadako Mother Comfessor,
 


U
Ulikuja hadi hapa Mwenge Moshi nikakupa pa kulala ushirikiane na wanachuo ukalalamika kuwa ni mbali kutokea mwenge kuenda kcmc kwa bajaji ...nikakutafutia chumba na nikakupa pesa ya kupanga karibu na ofisi niliyokukabidhi nikakupa na godoro la kuanzia

Ukanishauri tuanzishe biashara ya chipsi hapo nje ya steshenary wakati huu tulipokuwa tunasubiri wanachuo jumapili nikakuletea vitu vya kuchoma chipsi na mishikaki nikakupa na simu ya ofis maana kila mara unalalamika simu yako inakata chaji .

Jana nikaleta kijana ambae anapika chipsi na akapika nawe ili wewe umsimamie na pia usimamie steshenary maana wanachuo wamerudi jana
Leo asubui tumeamka ukanitumia sms na nikakupa maelekezo ya kazi za leo saa moja nakupigia simu umeniblock nilipokupigia na simu ya mtu mwingine nikajitambulisha ukatuma sms nilizobatisha kwenye huu uzi

Fedha za mauzo ya toka umeanza kazi jumatatu iliyopita hadi leo hujanipa mchanganuo wake ........na simu yangu hujanipa

Sawa wewe ni msomi sijui shida yako kubwa ilikuwa ni nini hasa .
Jirani ananipa funguo na anasema umekuja na bajaji ukakabidhi funguo ukamuambia unaenda kusimamia biashara zako
 
Duuuh makubwa haya!
 
Hiki ni nini🙄
 
Ginimbi mchezo?
 
"Hawezi kufanya kazi ya kuuza chips, yeye ni degree holder ana ndoto kubwa. Hizo kazi tafuta watu wa kawaida."

Huyu hajapigwa na maisha vile inavyotakiwa. Akiombe kazi hiko cheti kimlishe.
 
Huyu sio mwaminifu kabisa. Anazidi kujiharibia CV
hamna cha uaminifu ngoja nieleze kidogo huyo mama alinitafuta ndio tukazungumza vizuri akanambia niende moshi! nilichokifanya nikakopa hela ya nauli kwenda kwenye fursa aliyoniitia nilipokuwa safalin moshi mjini akanitumia namba za boda aje kunichukua yule boda nilovyofika tu nikampigia akaja stand akanichukua safali ikaanza kuelekea sehemu ambayo huyu mama alinielekeza ambapo ni maeneo ya ushirika wa neema pale kcmc tulivyofika nikamlipa yule boda hela yake then utambulisho ukaanza nikaelekezwa pahala pa kujihifadhi ile siku ambapo huyo mama ana nyumba yake ya wapangaji na ni wanafunzi wa chuo cha mwenge hivo kwa kuwa wengi wao walikua bado wapo likizo nikapewa chumba kimoja cha mpangaji nijistili kwa usiku huo ikiwa ni muda wa jion sijakaa sawa hata bila kupumzika nikaambiwa twende nikaoneshwe pahala pa kazi kwa kua nia yangu ni kazi nikamwambia madam twende tu hamna tabu hivo safali ikaanza kwenda maeneo ya chuo cha kcmc ambapo ndo kuna hilo eneo la kazi,
wakati tukiwa njian madam na mume wake wakashauliana kuwa lazima nikae karibu na eneo la kazi ili niwe nakawia kufunga nikawambia ni jambo jema mana tutapunguza gharama
punde tukawa tumefika eneo la kazi ambapo mimi ndo nilitakiwa kutoa plan ni vitu gani vinafanyikaga stationary ili avilete! basi kwa kuwa katika pita pita zangu na uzoefu wa stationary nikamshauri nini tufanye na akanipa moyo akasema kazi naiweza,
Changamoto ikaanza jion hiyo hiyo tukaanza kutafuta room maeneo ya kcmc ila tulifanikiwa kiasi na kiasi hatukufaniwa mana kwenye kufanikiwa tulipata room ila tukaambiwa bei ni 50000 ila tukaona ni gharama nikiwa mimi na mume wa huyo mama,basi hatukukata tamaa tukapelekwa sehem ingine room ya 30000 ila mazingira yake ya choo yakawa so mazuri binafsi sikupapenda na nikamwambia mume wa huyo dada kuwa mimi napenda sehemu safi haijalishi nipo katika hali ngumu kiasi gani huyo jamaa akanielewa hivo tukaachana na hiyo room tukarud ofisin ambapo tulikua tumemwacha madam tuluvyofika nikapewa maelekezo ya awali kama nilivyokwisha sema huko juu,nilitakiwa kusema plan nzima ya ofisi mana ndo kwanza tulikua tunaianzisha yako mengi ila nimeeleza hayo machache
Mwanzo wa vituko sasa
siku hiyo madam alinipa 5000 ya chakula mana ndo nilikua nimefika na nauli pia ya kurudia kule kwenye nyumba za wapangaji kiukwel mfukoni nilikua nimebakiwa na 1500 tsh hivo kwanza kwa kua nilikua mgeni na kagiza kalikua kameanza nikapanda bajaj kwa 500tsh nilivyofika ushorika wa neema nikashuka then kuna distance ya kutembea ili nifike hivo nikaamua kutembea yako mengi ila na summarise,
siku iliyofuata asubuhi nikawahi kazin sa moja hivi badae madam akaleta printers,pc scanner na vufaa vingine ila kwa bahat mbaya vilikua vmekaa mna mrefu havijafanya kazi ukabidi nishughulike navyo vyote hadi viwake wakat huo madam ameenda kazin kwake
nikapambana navyo almost siku nzima vikawaka vyote kasolo coloured printer ilokuwa nashida ya kimfumo
nikafanya maintenance vikakubali kuanza kuprint ila ptinter moja cartrige ink(wino)ukawa umeisha hivo ukatakiwa kubadilishwa wakat huo mi sikusafik na toolkit(vifaa vya kufungulia wala pc) mana madam alikua ashanieleza aina ya kazi ninayoenda kukutana nayo kabla na nyingine ikawa haina wino kabisa hivo badae nikampa feedback madam kua tunahitaji fundi printer aje atusaidie ili itoe huduma na akafanya hivo kweli hatimae kazi ikaanza
siku ilofata madam akaanza kunishaulu tuuze mihogo chipc mayai maziwa kuku kama alivyokua amepanga yeye mi nikamkubalia kwa kua nipo kwake ila sikupenda mana mana madam alinielekeza kuwa yeye atakuwa analeta vitu mi naviandalia hapo ofisini! yani ict officer nianze kuchemsha maziwa na kupima,,nimenye viazi nikaange chipc,nimenye mihogo nipike nichome mishikaki,ila kwa kuwa kum argue moja kwa moja nilikuwa nashindwa ikabidi nikubali ila roho inauma binafsi niseme ukweli niliona ni udhalilishaji na matumizi mabaya ya elimu yangu hata kama nina shida sio nianze kuchoma chipc,kuuza mihogo na kadharika na yalikuwa sio makubaliano yetu hayo kabla ya mimi kupanda bus,
Utata kwenye maradhi
baada ya siku kuwa zinaenda madam akajisahaulisha kuwa nilistiliwa kwenye chumba cha mtu ikabidi nianze kutafuta room na kumsisitizia ila aliishia kusema hana hela,
kuna siku nimepata room ya 30000tsh ambapo nilitakiwa kulipa 10000tsh kwanza madam alisema hana hela nifanye namna mimi mwenyewe kiukweli nikikwazika ila siku muoneshea hiyo hali mana aliniacha tumesimama mimi na mwenye nyumba ye akapanda gari akaondoka nikabaki na mbe mbeleza yule dada asikipangishe ila nikamkomalia madam akanipa 10000 nikaenda kulipa baada ya kulipa matandiko nayo yakawa kasheshe,madam akanijibu niafute godoro mwenyewe ye hana namna wakat huo akijua mimi ni mgeni hapa ndo niliona huyu mtu so mtu wa kawaida nikahisia kuona kuwa future yangu iko kubaya baadae baada ya kumlalamikia mana imefikia stage nauli sina natembea kwa mguu usiku kurud getoni hapa ndo nikajiona elim haijanisaidia kitu kwa changamoto nilizo ziona yako mengi ila ni hayo machache,
kula yangu ikawa shida;
kiukweli kuna siku nilikua naenda kibandani nauza 1400tsh na sina hela ya breakfast lunch wala dinner so nikawa napiga pass ndefu ili nione mwisho wa hayo maisha
Siku aliyo niudhi hadi kuondoka kiukweli nilikuwa nimepanga nimtengenezee mazingira kwanza then nimuage japo nilikua cjamwambia ni nin nafikilia ila una siku ameleta mihogo kama hot pot nzima ila ikanunuliwa ya 600tsh usiku alivyoanza kuniuliza hesabu na kumtajia mihogo nimeuza 600 na kuna vitu vingine waliuza afu akanuelekeza nitoe chenj then nilivyomueleza nimetoa chenji akanijibu vibaya hivo sikuwa na jinsi nilimuomba rafiki angu nauli nikaamka haraka nikaenda ofisin nikampa mtu funguo zake then nikaenda dar kwa hasira zangu na nika block mana sikutaka usumbufu
N.B
Madam wewe ni msomi na mfanyakazi just imagine vitu tulivyozungumza ndivyo nilivipata?? ok hata kama vilibadilika sawa sio mbaya,Lakin aina ya maisha uliyokuwa umenichagulia ni ya hali ya kawaida? au kwa sababu nilisema nina shida ndo ikabidi unichukulie hivo?
sina mengi ila kwa niliyo yaona nashauri kama una mtoto mpeleke shule apate uelewa wa kutosha aweze kuya mudu maisha yake!
Pia tujifunze kuheshim watu sio kwamba haimanishi kuwa hatujitambui ndo mana tukaanza kutafuta sehem ya kujishikiza
wengine kukaa bila kupambana naamin kuwa ni step za maisha ru na yatapita
#asante
 
"Hawezi kufanya kazi ya kuuza chips, yeye ni degree holder ana ndoto kubwa. Hizo kazi tafuta watu wa kawaida."

Huyu hajapigwa na maisha vile inavyotakiwa. Akiombe kazi hiko cheti kimlishe.
tunapotafuta sehemu za kujishikiza au kazi haimanishi tumepigika na maisha mkuu hilo sahau! nyie ndo mnatesa watoto wa watu kisa hawajiwezi never issue tunataka kusolve matatizo yaliyopo kwenye jamii.Umasikini wa akili unaanzia hapo mtu gani umesoma afu hata kujisimamia huwezi eti kisa "cheti kikupe ugali" kwenye maisha naamini nguvu ya elimu na nguvu ya pesa siwezi kukoswa pesa afu nikoswe na elimu nitakuwa sina utofauti na mtu ambae hana pumzi na ubongo.
 
Haya nenda maofisini kaombe kazi ndugu. Huko kwenye level zako.
 
Analalamika kwamba alikupa cm vp ulimrejeshea cm yake
 
daftari liko hapo la mauzo na kila kitu usitafute huruma soma daftari
 
We mtoto ni mpumbavu Sana.

Samahani lakini Bado una utoto mwingi sana. Duniani unapendwa na wewe tu. Narudia tena anaekupenda ni wewe. Wengine wote waliosalia wanapenda Thamani yako ( Value). Value ndio itakupa maisha na kuwa treated unavyotaka wewe. Ulichopaswa kufanya ni kuonesha value kiutendaji na sio maneno maneno. Kupitia value yako ungeshangaa unapewa hata mradi mwingine mkubwa kuliko huo unaouona wa kipumbavu.

Jifunze kuonesha Thamani yako kiutendaji. Hujawahi kuona watu wanajitolea ofisi mbalimbali Tena bure ??! Pale lengo Ni kuwapa nafasi watu waoneshe Value zao na baadae husjiriwa. Hakuna muajiri au mtu atakupa network kwa maneno yako ya huruma huruma, prove kwamba wewe ni wa thamani kubwa kiutendaji.


Kuna watu kupitia hizo kazi unazoziona za kijinga wamepata network za kazi either kupitia kwa wateja au mabosi. Mtu anafika hapo dukani anaona wewe ni wa Thamani and you deserve better anakupa kazi nyingine kubwa ila sio kwa maneno maneno tu na unavyojiona Bora.


Nilichojifunza bado una utoto mwingi, bado una akili za kichuo na ndoto za kipumbavu. Nakuhakikishia Kama usipobadirika hata ukipata kazi ya kuajiriwa nzuri hutadumu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…