Japo kuwa umri wako na bandiko lako vinanilazimisha nitoke nje ya mada, nikuhakikishie tu kuwa sitatoka nje ya maada,
Maoni yangu kwako ni kama ifuatavyo,
Kama kweli umedhamiria kutafuta mke na si demu, basi tumia njia ifuatayo, kama wewe ni mkazi wa Dodoma mjini jitahidi kila jumapili uwe unasali kwenye maeneo ambayo wanavyuo husali kwa wingi, baada ya hapo ongea na mchungaji amalize mambo,
Kama upo Dar jitahidi uwe unaenda kusali pale kawe kwenye kanisa la wasabato hapo kuna wanavyuo wengi husali hapo hii itakusaidia kupata mwenye degree kirahisi kabisa, wewe unachokifanya ni kuingia kiheshima moja moja kwa moja kuwa umemuona kwa muda mrefu unataka kumuoa, au tumia wachungaji.