ilisha juniour
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 714
- 219
natafuta mchumba ambaye ni tasa na ambaye atakuwa tyari tufunge ndoa baada ya kufahamiana,nipo kanda ya ziwa kikazi,umri miaka 30,elimu yangu ni chuo kipato cha wastani,napenda awe na umri kuanzia miaka 26 asizidi 35,awe amejiajiri ama kuajiriwa elimu kidato cha nne na kuendelea,mambo mengine tutawasiliana zaidi kwa pm,naomba kuwasilisha
Si dhan kama kuna atayejitokeza.
Wewe ni mfuasi mzuri wa dini?
Me nadhan ungenuliza ki vingine.
tasa? why? Isije ikawa na matasa wameanza kuwa dili kama albinos
umenichekesha sana kaka anyway ni mawazo yako piaMambo ya kanda ya ziwa yanatisha usikute masharti ya mganga hayo au unataka kumtoa sadaka bint wa watu,kuweni makin mabinti
wana haki pia ya kupendwa kaka,na kwakuwa nao ni binadamu nna imani ntampata
au ww ngumba ndo mana wataka tasa ili asikusumbue kuhusu mtoto?
kwa maana ipi?,
Hako ka ombi kako kama ki unyanyapaa flan hizi.
Ni kweli uwazi ni mzuri ila usingesema "Tasa" labda ungesema ambaye hapati mtoto
Nooo hiyo nayo haiko poa yn sijui ingetumika lugha gani
Ila hiyo uliyotumia ngumu sana.
Sijaelewa sehemu moja! Yaani kutokuwa na uzazi ni condition au wewe una matatizo ya uzazi kwahiyo unahitaji asiye na uzazi mwenzako ili pasiwe na unyanyapaa kati yenu?! Au may be una matatizo ambayo yanaweza kuhatarisha uhai wako endapo unashika ujauzito (am assuming ni mwanamke manake huja-specify)!wana haki pia ya kupendwa kaka,na kwakuwa nao ni binadamu nna imani ntampata
chukua aliyefika menopause, mbona simple tu.