Natafuta kiwanja

Natafuta kiwanja

Ngatelefijo

Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
20
Reaction score
3
Natafuta kiwanja maeneo ya Kibaha au mlandizi au kongowe . Yeyote aliyenacho tuwasiliane anipe mawasiliano
 
nenda halmashauri ya wilaya ya kibaha wana viwanja kibao
 
Natafuta kiwanja maeneo ya Kibaha au mlandizi au kongowe . Yeyote aliyenacho tuwasiliane anipe mawasiliano

Halmashauri ya wilaya na ya mji Kibaha zinauza viwanja bei zinatofautiana kuanzia 3500-6000 kwa sqm ukifika katija halmashauri hizo unaulizia ofisi ya ardhi utaelekezwa taratibu zote.. ila ukienda na passport size mbili, elfu kumi na copy ya kitambulisho unaweza punguza safari za kwenda na kurudi maana hivyo ukiwa navyo utaweza jaza fomu na kuiacha pamoja na kuchagua kiwanja.

Kama huhitaji vya kupima kuna mashamba yanauzwa Kongowe km6 kutoka barabarani wanauza Shs Mil 3 kwa heka...
Kwa mawasiliano unaweza nitaguta kwa 0684474188 nikupatie namba ya afisa ardhi wa wilaya zote hizo mbili
 
Nunua kiwanja maeneo ya Mbezi kwa Msuguri (Temboni, Msingwa) na Kifuru, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na ndugu Oswald Sh. Richard kwa simu namba :
00255784342632 au +255767342632
E-mail : cosiastore@yahoo.fr

1. Kiwanja cha kwanza kipo Mbezi kwa Msuguri, umbali wa kilomita tatu toka barabara ya Morogoro. Kiwanja hiki kipo kando ya barabara ya Msingwa ambayo ni ya changarawe na inapitika. Kina mita 30x40, pia kina nyumba ya vyumba viwili na baraza mbili. Nyumba hii ina umeme. Pia maji yanapatikana mita mia tatu toka kiwanjani. Bei yake ni Tshs. 55 milioni.

2. Kiwanja cha pili kipo Mbezi kwa Msuguri pia. Kuna umbali wa km 2 kutoka barabara ya Morogoro. Barabara ya kuelekea kiwanjani (maeneo ya mtaa wa Temboni) ni ya changarawe na inapitika. Kina ukubwa wa 1350M[SUP]2 [/SUP]
Kimepimwa na hati miliki yake ipo mbioni kutoka. Pia kina uzio wa waya. Bei yake ni Tshs. 60 milioni. Kuna maji umbali wa mita 200 kutoka kiwanjani. Umeme upo.

3. Viwanja vingine vipo eneo la Kinyerezi-Kifuru, umbali wa kilomita 1 toka barabara ya Kinyerezi-Mbezi. Hivi vipo viwanja 14. Vina ukubwa usio sawa.Vipo vya mita 22x25, 20x23, 27x23 na 20x20. Bei zake ni Tshs. 7 millioni kila kimoja. Eneo hili limefikiwa na mradi wa Serikali wa kuwekewa umeme, na wameshaweka nguzo ila bado kuweka nyaya na hatimaye kukamilisha mradi. Maji ya uhakikika kwa sasa ni kama umbali wa kilomita 2.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom