Natafuta kibalua

Tmatimba

Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
66
Reaction score
10
Habari wakuu,

Mimi ni mhitimu wa Stashahada ya Manunuzi na Ugavi(Diploma in Procurement and Supplies management),

Naishi Mbagala kwa mpili(saba saba) Temeke Dar,

Kwa yule yoyote anayetaka musaidizi wa muda mufupi au hata muda mrefu kulingana na makubaliano kwenye kitengo chochote niko tayari kufanya kazi kwa gharama yoyote ili muladi niweze kula na kushiba tu

Nasema kazi yoyote kwasababu kitengo Chetu cha Procurement imekuwa ngumu sana kupata nafasi hasa sie Diploma holders

Napatikana kwa

tmatimba2004@gmail.com

Niko tayari wakati wowote
 
Wewe Manunuzi na ugavi ndio uandikaji gani huu?? mbona unaandika Kiswahili cha ajabu hivi?? ni keyboard ina tatizo au wewe ndio tatizo?
 
Usikate tamaa endelea kumwomba Mungu siku moja utakanyaga kobe kichwa! Ila Kiswahili kwako inaelekea ni mgogoro! Hebu jaribu Kiingereza cha procurement tuone.
 
Jaribu kuomba kwenye hizi dispensary au hospitali za watu binafsi.
 

Hivi wahitimu wa nchi hii siku hizi wamekuwaje? Hata kuandika kitu kimashiko hawawezi..wewe sio wa kwanza..huo uandishi tu mtu anapoteza imani nawe, maana unaonekana hata hauko 'serious'!
 
Hivi wahitimu wa nchi hii siku hizi wamekuwaje? Hata kuandika kitu kimashiko hawawezi..wewe sio wa kwanza..huo uandishi tu mtu anapoteza imani nawe, maana unaonekana hata hauko 'serious'!

kwahiyo?
 
kibalua=kibarua.
mbagar =mbagala.
wewe ni msomi jaribu kuwa makini hata kama una haraka kiasi gani kwa siku hizi kuna usaili wa kuandika na kama una diploma na uandishi ni huu hata kama nafasi ziko 10 na usaili uko peke yako watakupiga chini tu.
 
Mshirikishe na Mungu pia endlea kutafuta sehem mbalimbali iko siku utafanikiwa.
 
samahini, kwani jinsia yako ni ipi? ke au me
 
Endelea kutafuta,naamini MUNGU hamtupi mja wake.utapata tu.
USHAURI: Utakapopata nafasi ya kusoma Shahada,soma B.B.A with education(Bachelor of Business Administration)with educ au B.Ed.Commerce. Utakuwa Multipurpose(wigo mpana)ktk ajira.kwa vile unapenda masomo ya biashara nadhani itakufaa,na unaweza ukafundisha vyuo vya biashara vilivyosajiliwa na NACTE ambavyo vinatoa Certificates,diploma etc.ingawa wengi wenu hampendi kusikia 'Education'lakini ni ajira pia.
 
Heshima kwako mkuu,

Ahsante.

Nimependa ushauri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…