Natafuta kazi!

Natafuta kazi!

MAANAX

Member
Joined
Dec 9, 2012
Posts
36
Reaction score
2
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 20 nimemaliza kidato cha nne mwaka jana ila sikuweza kuchaguliwa kuendelea, ninajua kuongea kingereza vizuri pia nina uwezo mkubwa katika hesabu na pia niko na uwezo mkubwa katika computer. Natafuta kazi ya kuuza dukani liwe la jumla au rejareja.
 
ungekuwa na unajua hesabu si ungefaulu hata kiswahili na civics
 
Pliz people,try being serious,mtu anatafuta kazi badala ya kumsaidia mnamkejeli,wenye uwezo wa kumsaidia pliz msaidieni na Mungu atawabariki
 
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 20 nimemaliza kidato cha nne mwaka jana ila sikuweza kuchaguliwa kuendelea, ninajua kuongea kingereza vizuri pia nina uwezo mkubwa katika hesabu na pia niko na uwezo mkubwa katika computer. Natafuta kazi ya kuuza dukani liwe la jumla au rejareja.
Usijali Mkuu, Endelea Kuomba Mungu Ipo Siku nawe Utapata pa kutokea, Usijali Maneno na Ugumu unaoupitia, zote ndo changamoto zenyewe za Maisha, Binafsi ningekushauri Utafute japo ka mtaji kadogo ujiajiri.

Najua Watu wanweza hoji wapi utaupata huo mtaji? Kubali kujiumiza japo kwa miezi 6 hivi, maana hata mimi nilipomaliza Chuo na mambo ya kazi yakawa bila bila, nilienda katika kampuni kubwa kubwa za ulinzi na nikafanya nao kazi kama mlinzi wa kawaida ingawa nna degree yangu ya uhasibu, lengo lilikuwa ni kutafuta mtaji na kupata chakula kidogo.

Kilichopo ni hivi hizi kampuni za ulinzi, kila siku anaacha mtu kazi na kila siku anaomba mwingine, hii hutokana na changamoto za kazi husika na malengo ya mtu mwenyewe.

Miongoni mwa kampuni ambazo angalau ka hela ni kadogo lakini kanatoka mwisho wa mwezi kweli ni K.K Security, Security Group na Ultimate Security. Pia Kuna Gruop 4 Security nao si wabaya, muhimu ujue unaanzia wapi na unatarajia nini.

Kila la kheri Mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom